Posts

Showing posts from May, 2022

1 Mwokozi umeokoa

1. Mwokozi umeokoa, Nimekuwa wako wewe. Damu imenisafisha; Sifa kwa mwana Kondoo. Utukufu, Aleluya! Sifa kwa Mwana Kondoo! Damu imenisafisha, Utukufu kwa Yesu!   2. Nilijitahidi sana Ila sikupata raha; Bali kwa kumtegemea Nilipata Baraka.   3. Daima namwegemea Damu ikifanya kazi, Nikioga kwa chemichemi Itokayo Mwokozi.   4. Sasa nimewekwa wakfu; Nitaishi kwako wewe: Fahari nashuhudia Ya wokovu wa bure.   5. Nasimama kwake Yesu, Ameponya roho yangu; Ameniondoa dhambi, Anifanye mzima.   6. Nilikuwa kifungoni, Niliteswa na dhambi, Nilifungwa minyororo Yesu akanifungua.   7. Sifa, ameninunua! Sifa, nguvu za wokovu! Sifa, Bwana huhifadhi! Sifa zake milele. 

2 Twamsifu Mungu

1. Twamsifu Mungu kwa Mwana wa Pendo, Aliyetufia na kupaa juu.   Aleluya! Usifiwe; Aleluya! Amin. Aleluya! Usifiwe, utubariki.    2. Twamsifu Mungu kwa Roho Mtukufu, Ametufunulia Mwokozi wetu.   3. Twamsifu Mwana, aliyetufia, Aliyetwaa dhambi akazifuta.   4. Twamsifu Mungu wa neema yote, Ametukomboa akatuongoza.   5. Tuamshe tena, tujazena pendo, Na moyoni uwashe moto wa Roho.

3 Hata ndimi elfu

1. Hata ndimi elfu elfu, Hazitoshi kweli Bwana Yesu kumsifu, Kwa zake fadhili.   2. Yesu, jina liwezalo Kufukuza hofu; Lanifurahisha hilo, Lanipa wokovu.   3. Jina hilo ni uzima; Ni afya amani; Laleta habari njema; Twalipiwa deni.   4. Yesu huvunja mapingu Ya dhambi moyoni; Msamaha, tena nguvu, Twapata rohoni.   5. Kwa sauti yake vile Wafu hufufuka Wakafurahi milele, Pasipo mashaka.   6. Ewe Yesu wangu Bwana, Uwezo nipewe, Kuhubiri kote sana, Wote wakujue.

4 Jina la Yesu, salamu!

1. Jina la Yesu, Salamu! Lisujudieni, Ninyi Mbinguni, hukumu Na enzi mpeni.   2. Enzi na apewe kwetu, Watetea dini; Mkuzeni Bwana wenu, Na enzi mpeni.   3. Enyi mbegu ya rehema, Nanyi msifuni; Mmeponywa kwa neema, Na enzi mpeni.   4. Wenye dhambi kumbukeni Ya msalabani, Kwa furaha msifuni, Na enzi mpeni.   5. Kila mtu duniani Msujudieni, Kote-kote msifuni, Na enzi mpeni.   6. Sisi na wao pamoja Tu mumo sifani, Milele sifa ni moja, Ni “Enzi mpeni.” 

5 Jina lake Yesu tamu

1. Jina lake Yesu tamu; Tukilisikia Hutupoza, tena hamu Hutuondolea.    2. Roho iliyoumia Kwalo hutibika, Chakula, njaani pia; Raha, tukichoka.    3. Jina hili ni msingi, Ngao, ngome, mwamba, Kwa hili napata wingi, Kwangu ni akiba.    4. Yesu, Mchunga, Rafiki Mwalimu, Kuhani, Mwanzo, Mwisho, Njia, Haki, Uzima kifoni.    5. Moyo wangu hauwezi, Kukusifu kweli, Ila sifa zangu hizi, Bwana zikubali.    6. Na utakaponiita, Kuja kwako Bwana, Huko kwako sitaacha Kukusifu sana. 

6 Baba, Mwana, Roho

1. Baba, Mwana, Roho, Mungu mwenye enzi, Kila tukiamka tunakuabudu Baba, Mwana, Roho, Mungu wa mapenzi, Ewe Utatu, tunakusifu.    2. Baba, Mwana, Roho, wakuaminio Wanakutolea shukrani zao Wanakusujudia malaika nao: Wewe u mwanzo, nawe u mwisho.    3. Baba, Mwana, Roho, sisi tu gizani, Utukufu wako hauoni kosa; U Mtakatifu, nawe u mapenzi, U peke yako, mwenzio huna.    4. Baba, Mwana, Roho, Mungu mwenye enzi, Ulivyoviumba vyote vyakusifu: Baba, Mwana, Roho, Mungu wa mapenzi Ewe Utatu, tunakusifu. 

7 Ni tabibu wa karibu

1. Ni tabibu wa karibu; Tabibu wa ajabu; Na rehema za daima; Ni dawa yake njema.   Imbeni, malaika, Sifa za Yesu Bwana; Pweke limetukuka Jina lake Yesu.   2. Hatufai kuwa hai, Wala hatutumai, Ila kweli yeye ndiye Atupumzishaye.   3. Dhambi pia na hatia Ametuchukulia; Twenendeni na amani Hata kwake Mbinguni.   4. Huliona tamu jina La Yesu Kristo Bwana, Yuna sifa mwenye kufa Asishindwe na kufa.   5. Kila mume asimame, Sifa zake zivume; Wanawake na washike Kusifu jina lake.   6. Na vijana wote tena, Wampendao sana Waje kwake wawe wake Kwa utumishi wake. 

9 Yesu kwetu ni rafiki

1. Yesu kwetu ni rafiki, Hwambiwa haja pia; Tukiomba kwa Babaye Maombi asikia; Lakini twajikosesha, Twajitweka vibaya; Kwamba tulimwomba Mungu Dua angesikia.   2. Una dhiki na maonjo? Una mashaka pia. Haifai kufa moyo, Dua atasikia Hakuna mwingine mwema Wa kutuhurumia; Atujua tu dhaifu; Maombi asikia.   3. Je, hunayo hata nguvu, Huwezi kuendelea, Ujapodharauliwa Ujaporushwa pia, Watu wange kudharau, Wapendao dunia, Hukwambata mikononi, Dua atasikia. 

8 Taji mvikeni

1. Taji mvikeni, Taji nyingi tena, Kondoo mwake kitini, Bwana wa mabwana; Nami tamsifu Alikufa kwangu, Ni mfalme mtukufu, Mkuu wa Mbingu.   2. Taji mvikeni Mwana wa bikira; Anazovaa kichwani Aliteka nyara; Shiloh wa wanabii, Mchunga wa watu, Shina na tanzu vya Yese, Wa Bethilehemu.   3. Taji mvikeni Bwana wa mapenzi; Jeraha zake ni shani Ni vito vya enzi, Mbinguni hakuna Hata malaika Awezaye kuziona Pasipo kushangaa. 

10 Usinipite!

1. Usinipite Mwokozi, Unisikie; Unapozuru wengine, Usinipite.   Yesu,Yesu, Unisikie; Unapozuru wengine, Usinipite.   2. Kiti chako cha rehema, Nakitazama; Magoti napiga pale, Nisamehewe.   3. Sina ya kutegemea, Ila Wewe tu; Uso wako uwe kwangu; Nakuabudu.   4. U Mfariji peke yako; Sina Mbinguni, Wala duniani pote, Bwana mwingine.

11 Nina haja nawe

1. Nina haja nawe Kila saa; Hawezi mwingine Kunifaa.   Yesu, nakuhitaji Vivyo kila saa! Niwezeshe, Mwokozi, Nakujia.   2. Nina haja nawe; Kaa nami, Na maonjo haya, Hayaumi.   3. Nina haja nawe; Kila hali, Maisha ni bure, Uli mbali.   4. Nina haja nawe, Nifundishe Na ahadi zako Zifikishe.   5. Nina haja nawe, Mweza yote, Ni wako kabisa Siku zote. 

13 Tafuta daima utakatifu

1. Tafuta daima utakatifu; Fanya urafiki na Wakristo tu; Nena siku zotena Bwana wako, Baraka uombe kwa kila jambo.   2. Tafuta daima utakatifu; Uwe peke yako ukimwabudu; Ukimwangalia mwokozi wako, Utabadilishwa kama alivyo.   3. Tafuta daima utakatifu; Kiongozi wako aew Yesu tu; Katika furaha au huzuni Dumu kumfuata Yesu Mwokozi.   4. Tafuta daima utakatifu; Umtawaze Roho moyoni mwako; Akikuongoza katika haki, Hufanywa tayari kwa kazi yake. 

12 Ewe Roho wa Mbinguni

1. Ewe Roho wa Mbinguni Uje kwetu sasa. Ufanye makazi yako Ndani ya Kanisa.   2. Ndiwe mwanga, umulike Tupate jikana; Mengi kwetu yapunguka, Tujalize, Bwana.   3. Ndiwe Moto, teketeza Taka zetu zote: Moyo na iwe sadaka Ya Mwokozi, yote.   4. Ndiwe Umande, na kwako Tutaburudika, Nchi kavu itakuwa Ni yenye Baraka.   5. Roho wa Mbinguni uwe Nasi hapa chini, Mwili uufananishe Na kichwa Mbinguni. 

14 Yesu kwa imani

1. Yesu kwa imani, Nakutumaini, Peke yako; Nisikie sasa, Na kunitakasa, Ni wako kabisa Tangu leo.   2. Nipe nguvu pia Za kusaidia Moyo wangu; Ulikufa wewe, Wokovu nipewe Nakupenda wewe, Bwana wangu.   3. Hapa nazunguka Katika mashaka, Na matata; Palipo na giza Utaniongoza Hivi nitaweza Kufuata.   4. Takuwa mzima Nivushe salama Mautini; Sina hofu kamwe Ukiwapo nami Nami nikwandame Siku zote. 

15 Cha kutumaini sina

1. Chakutumaini sina Ila damu yake Bwana, Sina wema wa kutosha Dhambi zangu kuziosha;   Kwake Yesu nasimama, Ndiye mwamba: ni salama Ndiye mwamba: ni salama.   2. Njia yangu iwe ndefu Yeye hunipa wokovu; Mawimbi yakinipiga Nguvu zake ndiyo nanga.   3. Damu yake na sadaka Nategemea daima, Yote chini yakiisha Mwokozi atanitosha.   4. Nikiitwa hukumuni, Rohoni nina amani Nikivikwa haki yake Sina hofu mbele zake. 

16 Kumtegemea Mwokozi

1. Kumtegemea Mwokozi, Kwangu tamu kabisa; Kukubali neno lake Nina raha moyoni.   Yesu,Yesu namwamini, Nimemwona thabiti; Yesu,Yesu,yu thamani, Ahadi zake kweli.    2. Kumtegemea Mwokozi, Kwangu tamu kabisa, Kuamini damu yake Nimeoshwa kamili.   3. Kumtegemea Mwokozi, Kwangu tamu kabisa, Kwake daima napata Uzima na amani.   4. Nafurahi kwa sababu Nimekutegemea; Yesu,Mpendwa na Rafiki Uwe nami dawamu. 

17 Namwandama Bwana

1. Namwndama Bwana kwa alilonena Njia yangu huning’azia; Nikimridhisha atanidumisha Taamini nitii pia.   Amini utii, njia pweke ni hii Ya furaha kwa Yesu: amini ukatii.  2. Giza sina kwangu wala hata wingu Yeye mara huviondoa Woga, wasiwasi, sononeko, basi; Huamini nitii pia.   3. Masumbuko yote, sikitiko lote; Kwa mapenzi hunilipia; Baa, dhara, dhiki, vivyo hubariki Taamini nitii pia.   4. Mimi sitajua raha sawasawa Ila yote Yesu kumpa; Napata fadhili na radhi kamili, Taamini nitii pia.   5. Nitamfurahia na kumtumaini, Majumbani na njia-njia; Agizo natenda, nikitumwa hwenda, Huamini nitii pia. 

18 Akifa Yesu nikafa naye

1. Akifa Yesu nikafa naye Uzima upya huishi naye; Humtazama mpaka nje: Nyakati zote ni wake yeye.   Nyakati zote nimo pendoni, Nyakati zote ni uzimani, Humtazama hata atokee, Nyakati zote mimi ni wake.   2. Vita sipigi visivyo haki, Na Bwana wangu hapiganiki; Beramu yake haitwaliki, Napo po pote hila sitaki.   3. Sina mashaka, akawa mbali; Mizigo yote aihimili; Ananituliza Imanweli, Nyakati zote mimi husali.   4. Sina huzuni na mimi sidhii; Simwagi chozi, wala siguni; Sikuti afa, ila kitini Daima hunifikiri mimi.   5. Kila unyonge huusikia; Kila ugonjwa kwake hupoa; Yesu ni mwenye kuniokoa Nyakati zote hunijalia. 

19 Ndiyo dhamana, Yesu wangu

1. Ndiyo dhamana, Yesu wangu; Hunipa furaha za Mbingu; Mrithi wa wokovu wake Nimezawa kwa Roho yake.    Habari njema, raha yangu Yesu ndiye Mwokozi wangu, Habari njema, raha yangu Yesu ndiye mwokozi wangu.    2. Kumsalimu moyo wangu, Mara namwona raha yangu; Aniletea malaika, Wananilinda, taokoka.    3. Sina Kinyume, nashukuru, Mchana kutwa huja kwangu; Usiku kucha kuna nuru; Mwokozi wangu; ndimi huru.    4. Hali na mali anitwaa! Mara namwona anifaa, Nami nangoja kwa subira; Akiniita, nije mara. 

20 Ninaye rafiki naye

1. Ninaye Rafiki naye Alinipenda mbele; Kwa kamba za pendo zake Nimefungwa milele; Aukaza moyo wangu, Uache mageule, Mimi wake, yeye wangu; Ndimi naye milele.    2. Ninaye rafiki ndiye Aliyenifilia; Alimwaga damu yake Kwa watu wote pia; Sina kitu mimi tena, Nikiwa navyo tele; Pia vyote ni amana Ndimi wake milele.   3. Ninaye rafiki naye Uwezo amepewa; Atanilinda mwenyewe, Juu tachukuliwa; Nikitazama Mbinguni, Hupata nguvu tele; Sasa natumika chini, Kisha juu milele.   4. Ninaye rafiki naye, Anao moyo mwema; Ni mwalimu, kiongozi, Mlinzi wa daima; Ni nani wa kunitenga Na mapenzi ya mbele? Kwake nimetia nanga, Ndimi wake milele. 

21 Roho yangu hima

1. Roho yangu hima, na taa yako Kaiwashe vyema, hapa si pako; Nguvu zote pia za duniani Hazitakudhuru ukiamini.   Yesu yuko mbele, Yesu yu nyuma, Yesu vivyo kando, walindwa vyema.   2. Adui shetani, na nguvu zake, Bwana ameshinda, kwa kifo chake; Wewe nguvu huna, huna kabisa, Ndiwe mpungufu, mnyonge hasa.   3. Toka na mapema, mbele ya wote, Omba, bisha sana, maisha yote; Vita vikaliko, macho ukae, Jivike silaha, nawe sishindwe.   4. Bwana Yesu ndiye kwako mchunga, Neno lake Bwana ndilo upanga; Mbingu zitakwisha, na nchi pia, Neno lake Bwana laendelea. 

22 Kale nilitembea

1. Kale nilitembea Nikilemewa dhambi Nilikosa msaada, kuniponya mateso.    Usifiwe Msalaba! Lisifiwe kaburi! Linalozidi yote, Asifiwe Mwokozi!    2. Hata nilipofika, Mahali pa Msalaba, Palinifaa sana, Sitasahau kamwe.   3. Hicho ndicho chanzo, Cha kufurahi kwangu. Hapo ndipo mzigo, Uliponituliwa.   4. Panapo msalaba, Kinatolewa cheti, Cha kuingia Mbinguni, Kisicho cha kanisa.   5. Yule Bwana mjinga, Likwenda bila cheti, Kitumai kwingia, Kama walio nacho.   6. Lipofika langoni, Akaulizwa cheti, Cha kumwonyesha Bwana, Akakutwa hanacho.   7. Lituhuzunishalo, Ni ninyi msio nacho, Kuwa kama mjinga, Kwa siku ya arusi!   8. Ubavuni mwa Yesu, Mlitokea damu, Chemchemi ya uzima, Itakasayo roho.   9. Jitahidi wingie, Damuni mwa Mwokozi, Utafutiwa dhambi, Toka rohoni mwako. 

23 Ni salama rohoni mwangu

1. Nionapo amani kama shwari, Ama nionapo shida; Kwa mambo yote umenijulisha, Ni salama rohoni mwangu.    Salama rohoni, Ni salama rohoni mwangu.    2. Ingawa shetani atanitesa, Nitajipa moyo kwani Kristo ameona unyonge wangu, Amekufa kwa roho yangu.   3. Dhambi zangu zote, wala si nusu, Zimewekwa msalabani; Wala sichukui laana yake, Ni salama rohoni mwangu.   4. Ee Bwana himiza siku ya kuja, Panda itakapolia; Utakaposhuka sitaogopa Ni salama rohoni mwangu.

24 Mwokozi moyoni mwangu

1. Tangu siku hiyo aliponijia, Akae moyoni mwangu, Sina giza tena, ila mwanga pia Kwa Yesu mwokozi wangu.    Amani moyoni mwangu, kwa Yesu, Mwokozi wangu; Sina shaka kamwe, Kwa sababu yeye, Yu nami moyoni mwangu.    2. Sina haja tena, ya kutanga-tanga, Ndiye kiongozi wangu. Dhambi zangu zote zimeondolewa, Na Yesu, Mwanawe Mungu.   3. Matumaini yangu ni ya hakika, Katika Mwokozi wangu. Hofu zangu na hamu zimeondoka, kwa kuwa ninaye Yesu.   4. Siogopi tena, nikiitwa kufa, Yu nami daima, Yesu. Mlango wa Mbinguni ni yeye pia, “Tapita humo kwa damu.”   5. Nitaketi na yeye huko milele, Nisifu Mwokozi wangu. Nina raha moyoni majira yote, Kwa Yesu, Mwanawe Mungu. 

25 Nimekombolewa na Yesu

1. Nimekombolewa na Yesu Aliyenirehemia; Kwa bei ya mauti yake Nimekuwa mtoto wake.    Kombolewa! Nakombolewa na damu; Kombolewa! Mimi mwana wake kweli.    2. Kukombolewa nafurahi, Kupita lugha kutamka; Kulionyesha pendo lake, Nimekuwa mtoto wake.   3. Nitamwona uzuri wake, Mfalme wangu wa ajabu; Na sasa najifurahisha, Katika neema yake.   4. Najua taji imewekwa Mbinguni tayari kwangu; Muda kitambo atakuja, Ili alipo, niwepo. 

27 Mungu ni pendo

1. Mungu ni pendo, apenda watu; Mungu ni pendo, anipenda Sikilizeni furaha yangu, Mungu ni pendo, anipenda.   2. Nilipotea katika dhambi, Nikawa mtumwa wa shetani.   3. Akaja Yesu kuniokoa, Yeye kanipa kuwa huru   4. Sababu hii namtumikia, Namsifu yeye siku zote. 

26 Yesu unipendaye

1. Yesu unipendaye Kwako nakimbilia, Ni wewe utoshaye, Mwovu akinijia; Yafiche ubavuni, Mwako maisha yangu; Nifiikishe mbinguni Wokoe moyo wangu.    2. Ngome nyingine sina; Nategemea kwako. Usinitupe Bwana , Nipe neema yako, Ninakuamania Mwenye kuniwezesha; Shari wanikingia, Vitani wanitosha.   3. Nakutaka Mpaji Vyote napata kwako; Niwapo muhitaji, Utanijazi vyako; Nao waangukao Wanyonge wape nguvu; Poza wauguao, Uongoze vipofu.   4. Bwana umeniosha Moyo kwa damu yako; Neema ya kutosha Yapatikana kwako; Kwako Bwana naona Kisima cha uzima; Mwangu moyoni Bwana, Bubujika daima. 

28 Anipenda ni kweli

1. Anipenda ni kweli; Mungu anena hili; Sisi wake watoto; kutulinda si zito.    Yesu anipenda, Yesu anipenda, Kweli anipenda, Mungu amesema.    2. Kwa kupenda akafa Niokoke na kufa; Atazidi taka, Sana ataniweka.   3. Anipenda kabisa; Niuguapo sasa Anitunza Mbinguni Nniliyelala chini.   4. Kunipenda haachi, Tu sote hapa chini Baada ya mashaka Kwake tanipeleka. 

29 Baba yetu aliye Mbinguni

1. Baba yetu aliye Mbinguni Amenifurahisha yakini Kuniambia mwake chuoni Ya kuwa nami Yesu pendoni.    Anipenda Mwokozi Yesu, Anipenda, anipenda; Anipenda Mwokozi Yesu, Anipenda mimi.    2. Nimuachapo kutanga mbali, Yeye yu vivyo, hupenda kweli, Hunirejeza kwake moyoni; Kweli yu nami Yesu pendoni.   3. Anipenda! Nami nampenda; Kwa wokovu alionitenda; Akanifia Msalabani Kwa kuwa nami Yesu pendoni.   4. Haya kujua yanipa raha; Kumuamini kuna furaha; Humfukuza mara shetani, Kwona yu nami Yesu Pendoni.   5. Sifa ni nyingi asifiwazo, Moja ni sana katika hizo, Wala siachi, hata Mbinguni, Kwimba, “Yu nami Yesu pendoni”.