Posts

Showing posts from February, 2022

100 Tumrudie Bwana

1. Mbona washangaa njiani? Mbona warejea nyuma? Warudi tena gizani Alimokutoa Bwana?    2. Ni ya bure yote haya, Uliyofunzwa ya Mungu? Ni bure amekufia Bwana Yesu kwa uchungu?   3. Wamtia kristo aibu Na maneno yake pia? Siku yaja ya hesabu, Utamjibuje Bwana?   4. Upandapo tena hayo, Halafu utayavuna. Rudi kwa Bwana upesi, Mwombe akupokee tena. 

101 Twonane milele

1. Nyimbo na tuziimbe tena Za alivyotupenda mbele; Kwa damu ya thamani sana! Mbinguni twonane milele.    Twonane milele, Twonane bandarini kule; Twonane milele, Twonane bandarini kule.    2. Hupozwa kila aoshwaye, Kwa damu ya Kondoo yule; Ataishi afurahiye Vya Yesu mbinguni milele.   3. Hata sasa hufurahia Tamu yake mapenzi yale, Je, kwake tukifikilia, Kutofarakana milele?   4. Twende mbele kwa jina lake, Hata aje mwokozi yule, Atatukaribisha kwake, Tutawale naye milele.   5. Sauti zetu tuinue Kumsifu Mwokozi yule, Ili watu wote wajue Wokovu u kwake milele. 

102 Kazi yangu ikiisha

1. Kazi yangu ikiisha, nami nikiokoka; Na kuvaa kutokuharibika, Nitamjua Mwokozi nifikapo ng’amboni; Atakuwa wa kwanza kunilaki.   Nitamjua, nitamjua, nikimwona uso kwa uso; Nitamjua, nitamjua, kwa alama za misumari.    2. Furaha nitapata nikiona makao Bwana aliyotuandalia; Nitamsifu mwokozi kwa rehema na pendo Vilivyonipa pahali Mbinguni.   3. Nao waliokufa katika Bwana Yesu, Nitawaona tena huko juu; Lakini nifikapo kwake huko Mbinguni, Nataka kumwona Mwokozi kwanza.   4. Milangoni mwa mji Bwana atanipitisha, Pasipo machozi wala huzuni. Nitauimba wimbo wa milele; lakini Nataka kumwona Mwokozi kwanza. 

103 Kaa nami

1. Kaa nami, ni usiku tena; Usiniache gizani, Bwana; Msaada wako haukomi; Nili peke yangu, kaa nami.    2. Siku zetu hazikawi kwisha, Sioni la kunifurahisha; Hakuna ambacho hakikomi, Usiye na mwisho kaa nami.   3. Nina haja nawe kila saa; Sina mwingine wa kunifaa; Mimi nitaongozwa na nani Ila wewe? Bwana, kaa nami.   4. Sichi neno uwapo karibu; Nipatalo lote, si taabu; Kifo na kaburi haviumi; Nitashinda kwako, kaa nami.   5. Nilalapo nikuone wewe, Gizani mote nimulikiwe; Nuru za mbinguni hazikomi, Siku zangu zote kaa nami. 

104 Twasoma ni njema sana

1. Twasoma, ni njema sana Mbinguni, kwa Bwana; Twasoma, dhambi hapana, Mbinguni kwa Bwana; Malaika wema wako, Vinanda vizuri viko, Na majumba tele yako, Mbinguni kwa Bwana.    2. Siku zote ni mchana, Ni nchi ya raha; Wala machozi hapana, Ni nchi ya raha; Walioko wanuona Uso wa Mwokozi, tena Jua jingine hapana, Ni nchi ya raha.   3. Nyama na vitu viovu Havimo kabisa; Kifo nacho, na ubovu, Havimo kabisa. Ni watakatifu wote, Wameoshwa dhambi zote; Wasiosafiwa wote Hawamo kabisa.   4. Tuna dhambi, pia sote, Mwokozi akafa; Kwake tutaoshwa zote, Mwokozi akafa; Kwake twapata wokovu, Tutawona utukufu; Mbinguni tutamsifu; Mwokozi akafa.   5. Baba, mama, ndugu zetu, Twendeni kwa Bwana; Huku chini sio kwetu, Twendeni kwa Bwana; Tusishikwe na dunia, Na dhambi kutulemea; Tutupe vya chini pia, Twendeni kwa Bwana. 

105 Kuwatafuta

1. Kuwatafuta wasioweza, Kuomba wamrejee Yesu, Kuwaambia maneno yake, “Njooni kwangu, nawapenda”.    Nitakwenda, (kwenda), niwatafute Waongofu (wa Bwana) wageuke, Waingie (wote) katika zizi La Mkombozi (wetu) Yesu kristo.    2. Kuwatafuta wasioweza, Waonyeshwe Mwokozi wetu, Kuwaongoza, wapate wote Uzima wa milele.   3. Kazi hiyo nataka kufanya, Leo nimesikia mwito Kuwainua waangukao, Waletwe kwake Yesu njia.

106 Mungu awe nanyi daima

1. Mungu awe nanyi daima, Hata twonane ya pili, Awachunge kwa fadhili, Mungu awe nanyi daima.    Hata twonane huko juu, Hata twonane kwake kwema; Hata twonane huko juu, Mungu awe nanyi daima.    2. Mungu awe nanyi daima; Ziwafunike mbawaze, Awalishe, awakuze; Mungu awe nanyi daima.   3. Mungu awe nanyi daima; Kila wakati wa shani Awalinde hifadhini; Mungu awe nanyi daima.   4. Mungu awe nanyi daima; Awabarikie sana, Awapasulie kina; Mungu awe nanyi daima.

107 Ewe Baba wa Mbinguni

1. Ewe, Baba wa Mbinguni, Usikie twombalo Hapa chini duniani, Na uwe radhi nalo   Ee Mungu, bariki Ndugu hawa wawili! Ee Mungu, bariki Ndugu hawa wawili!   2. Watu hawa mbele zako, Na mbele ya kanisa; Watimize Neno lako Wanakutana sasa.   3. Kama Yesu na Kanisa, Ni mmoja, na hivyo, Watu hawawape sasa Wawe mmoja vivyo   4. Walinde, Bwana, daima, Wabariki nyumbani Uwape nyingi salama Humu ulimwenguni.   5. Wabariki, ewe Bwana, Watu hawa wawili, Wape upaji wa wana, Wafurahishwe kweli.   6. Siku za duniani Zitakapopungua, Wape kurithi Mbinguni Mema ya kwendelea.

108 Twenenda sayuni

1. Mpendao Bwana Ije raha yenu! Imbeni nyimbo za raha Wa ibada yenu.    Twenenda Sayuni, Mji mzuri Sayuni; Twenenda juu Sayuni Ni maskani ya Mungu.    2. Wasiimbe wao wasioamini, Watoto wa Mungu ndio waimbao chini.   3. Twaona rohoni Baraka za Mungu, Tusijafika Mbinguni Kwenye utukufu.   4. Tutakapo mwona Masumbuko basi, Huwa maji ya uzima, Anasa halisi.   5. Tupaaze sauti, Na fute machozi, Twenenda kwa Imanweli Naye ni Mwokozi.

109 Nitaimba ya Yesu

1. Nitaimba ya Yesu, Kwa rehema zake, Baraka nyingi sana Nimepata kwake; Nitaimba ya Yesu, Sadaka ya Mungu, Alimwaga damu Ukombozi wangu.   2. Nitaimba ya Yesu Hapa siku zote, Nitakapokumbuka Vyema vyake vyote; Nitaimba ya Yesu Hata mashakani, Yeye atanilinda Mwake ubavuni.   3. Nitaimba ya Yesu Niwapo Njiani; Takaza Mwendo, hata Nifike Mbinguni; Nikiisha ingia Mlangoni mle, Yesu nitamwimbia Mbinguni milele.

110 Mapya ni mapenzi hayo

1. Mapya ni mapenzi hayo, Asubuhi tunayo, Saa za giza hulindwa Kwa uzima kuamshwa.   2. Kila siku, Mapya pia Rehema, wema, na afya, Wokofu, na msamaha, Mawazo mema, furaha.   3. Tukijitahidi leo Na mwendo utupasao, Mungu atatueleza Yatakayompendeza.   4. Mambo yetu ya dunia Mungu atayang’aria, Matata atageuza Yawe kwetu ya Baraka.   5. Yaliyo madogo, haya Mungu tukimfanyia, Yatosha: tutafaidi Huvuta kwake zaidi.   6. Ewe Bwana, siku zote, Tusaidie kwa yote: Mwendo wetu wote vivyo, Uwe kama tuombavyo.

111 Neno lako Bwana

1. Neno lako, Bwana, Ni imara sana; Lilo latwongoza, Lilo latufunza.   2. Adui wabaya Wakikaribia, Neno lake Bwana Ni ulinzi sana.   3. Siku za dhoruba Soma ukiomba; Neno lake Bwana Msaada sana.   4. Ukiliamini, Hwenda na amani; Una na furaha Neno ni siraha.   5. Ni furaha kweli, Na wingi wa mali, Neno lake Bwana Kwa wasiokana   6. Neno la rehema, Tukali wazima; Faraja I papo, Tufarikanapo.   7. Tulijue sana Neno lako, Bwana, Hapa tukupende, Kisha kwako twende.

112 Nilikupa wewe maisha yangu

1. Nilikupa wewe Damu ya moyoni, Ili wokolewe, Winuke ufuni: Nimekunyimani? Umenipa nini?   2. Nilikupa miaka Yangu duniani Upate inuka, Kuishi Mbinguni: Nimekunyimani? Umenipa nini:   3. Niliacha nuru Za Baba, Mbinguni, Kwingia taabu Za ulimwenguni: Nimekunyimani? Umenipa nini?   4. Niliteswa sana, Mateso kifoni, Usije yaona Hayo ya motoni: Nimekunyimani? Umenipa nini?   5. Nimekuletea Huku duniani Upendo na afya Zatoka Mbinguni: Nimekunyimani? Umenipa nini?   6. Nipe siku zako, Udumu mwangani; Na taabu yako, Wingie rahani Nafsi, pendo, mali, Twae Imanweli.

113 Ni mfalme wa mapenzi

1. Ni Mfalme wa mapenzi Ndiye anichungaye, Sipungukiwi, hawezi. Kunipoteza yeye.   2. Kando ya mji mazima Yeye huniongoza Katika malisho mema Daima hunilaza.   3. Mara nyingi hupotea Kwa ukaidi wangu, Naye huniandamia, Hunirudisha kwangu.   4. Uvulini mwa mauti, Siachi hatari kamwe, Wewe Bwana huniachi, Mwokozi wangu wewe.   5. Waniandikia meza Neema kwako tele. Kwa wewe, yote naweza. Na msalaba mbele.   6. Kamwe hautapungua Uule wema wako; Mwisho, atanichukua, Juu, niimbe kwako.

114 Bwana Mungu, nashangaa kabisa

1. Bwana Mungu, nashangaa kabisa Nikitazama kama vilivyo Nyota, ngurumo, vitu vingi vyote viumbwavyo kwa uwezo wako. Roho yangu na ikuimbie Jinsi Wewe ulivyo Mkuu, Roho yangu na ikuimbie Jinsi Wewe ulivyo Mkuu.    2. Nikitembea pote duniani, Ndege huimba, nawasikia, Milima hupendeza macho sana, Upepo nao nafurahia.    3. Nikikumbuka kama Wewe Mungu Ulivyompeleka Mwanao, Afe azichukue dhambi zetu, Kuyatambua ni vigumu mno.    4. Yesu Mwokozi utakaporudi Kunichukua kwenda Mbinguni, Nitashukuru na kwimba milele, Wote wajue jinsi ulivyo. 

115 Kilima kando ya Mji

1. Kilima kando ya mji Alikufa Bwana; Kuokoa wakosaji Akateswa sana.   2. Kabisa hayasemeki, Mateso dhaifu Alikufa mwenye Haki Tupate wokovu.   3. Alimwaga damu yake Ili tuwe wema, Tufae kukaa kwake Mbinguni daima.   4. Hatuna mwenye imani Aliye na haki, Wa kutosha yetu deni, Rafiki Yesu tu.   5. Alijua peke yake Kufungu Mbingu Ufunguo damu yake Kondoo wa Mungu.   6. Aliyetupenda hivyo Nasi tumpende, Tukamtumai vivyo Na kazi tutende.

116 Bwana , U sehemu yangu

1. Bwana u sehemu yangu, Rafiki yangu wewe; Katika safari yangu Tatembea na wewe; Pamoja na wewe, Pamoja na wewe, Katika safari yangu Tatembea na wewe.    2. Mali hapa sikutaka, Ili niheshimiwe, Na yanikute mashaka Sawa sawa na wewe, Pamoja na wewe, Pamoja na wewe, Heri nikute mashaka Sawasawa na wewe.   3. Niongoze safarini, Mbele unichukue Mlangoni kwa Mbinguni Niingie na wewe. Pamoja na wewe, Pamoja na wewe, Mlangoni kwa mbinguni, Niingie na wewe.

117 Tufani inapovuma

1. Tufani inapovuma Sana moyoni mwangu, Huona pa kujificha Mkononi mwa Mungu.    Hunificha, hunificha Adui hatanipata, Hunificha, hunificha, Mkononi mwake.    2. Pengine kuna taabu Yanisongeza kwake; Naijua si hasira, Ni ya mapenzi yake.   3. Adui wakiniudhi Nami nikisumbuka, Mungu atavigeuza Vyote viwe baraka.   4. Niishipo duniani Ni tufani daima, Anilindapo rohoni Nitakaa salama.

118 Ni ujumbe wa Bwana

1. Ni ujumbe wa Bwana, Aleluya! wa maisha ya daima, Amenena mwenyewe, Aleluya! Utaishi ukitazama.   Tazama, ishi sasa! Kumtazama Yesu, Amenena mwenyewe, Aleluya! Utaishi ukitazama.   2. Ni ujumbe wa wema, Aleluya! Nawe shika, rafiki yangu! Ni habari ya raha Aleluya! Mwenye kuinena ni Mungu.   3. Uzima wa daima,Aleluya ! Kwake Yesu utauona. ukimtazama tu, Aleluya! Wokovu u pweke kwa Bwana.

119 Si damu ya nyama

1. Si damu ya nyama Iliyomwagika Iwezayo kuondoa Dhambi za wakosa.    2. Yeye Bwana Yesu Sadaka ya Mungu, Mwenye damu ya thamani, Ni mwokozi kweli.   3. Kwa imani yangu, Namshika yeye, Naziweka dhambi zangu Juu ya kichwa chake.   4. Mzigo wa dhambi Sichukui tena, Ameuchukua yeye, Juu ya msalaba.   5. Bwana Yesu ndiye, Mwokozi wa kweli Tumsifu siku zote, Twapata uhuru.

120 Enyi wanadamu

1. Enyi wanadamu mbona Sana mwatanga-tanga, Kama kondoo wanyonge, Wasio na mchunga? Yuko mchunga mmoja Mwenye mapenzi mema; Haya kutaneni kwake, Atawachunga vyema.    2. Mungu tunamwona kuwa Mwenye uwezo wote; Na nguvu zake zapita Mawazo yetu yote: Ni Baba,mapenzi yake Ni makubwa hakika; Hatuwezi kuyajua, Na hayana mpaka.   3. Rehema za Mungu nazo Zina upana sana; Kama huo wa bahari, Mwisho wake hapana; Haki yake ina mema, Kwa hayo twashukuru, Kwetu uko msamaha, Furaha na uhuru.   4. Mapenzi yake mapana, Sisi hatuna cheo Cha kutosha, nao moyo Una wema upeo; Ukombozi mwingi mno Katika damu yake; Sote twapata furaha, Kwa maumivu yake.    5. Yesu mkaribieni Njoni msife myoyo; Njoni kwake kwa imani, Mema yake ni hayo; Heri tuwe kama wana Tushike neno lake, Daima atujaza Tele furaha yake.

121 Liko lango moja wazi

1. Liko lango moja wazi, Ni lango la mbinguni; Na wote waingiao Watapata nafasi.    Lango ndiye Yesu Bwana Wote waingie kwake, Lango! Lango La Mbinguni ni wazi.   2. Yesu ndiye lango hili, Hata sasa ni wazi, Kwa wakubwa na wadogo, Tajiri na maskini.   3. Hili ni lango la raha, Ni lango la rehema; Kila mtu apitaye Hana majonzi tena.   4. Tukipita lango hili Tutatua mizigo, Tuliochukua kwanza, Tutavikwa uzima.   5. Hima ndugu tuingie Lango halijafungwa, Likifungwa mara moja Halitafunguliwa.

122 Bwana Yesu

1. Bwana Yesu, Bwana Yesu, Mbona unaumia? Unateseka sana, Kwa ajili ya kuomba, Waomba na jasho jingi likageuka damu.    Kumbe! Ni dhambi zangu zinazokuumiza. Bwana wangu, Mungu wangu, Mimi leo, naja kwako Ili niziungame.    2. Bwana Yesu, Bwana Yesu, Mbona unaumia, na mizigo mizito? Umejitwalia wewe, msalaba mabegani Kwa ajili ya watu.   3. Bwana Yesu, Bwana Yesu, Mbona unatukanwa, wawambwa kama mwizi, Bila kosa ukalia, Baba yangu, wasamehe, Chukua roho yangu.   4. Bwana Yesu, Bwana Yesu, Muda ulipofika, nchi ikawa giza, Mbinguni pakatulia, Angani pakawa kimya, Watu wakaogopa.   5. Bwana Yesu, Bwana Yesu, Jinsi ulivyoumwa, ukamwomba Baba, Leo umeshinda kifo, sasa wapaa Mbinguni, Naimba, Haleluya.

123 Nimeketi mimi nili kipofu

1. Nimeketi mimi nili kipofu Gizani nangojea macho; Ewe Bwana Yesu mwenye wokovu, Ondoa dhambi zangu nzito. Huruma hakuna aonaye, Gizani nagojea macho, Sasa nitakase nikusihiye, Yesu, na dhambi zangu nzito.    2. Tangu siku nyingi nimepofuka Natamani uso nikwone; Ewe Bwana Yesu, mwenye baraka Sema neno, basi, nipone.   3. Nimeketi mimi nili na giza, Nami ya kutumai sina; Ili nasikia kunong’oneza, “Kwake Yesu kuna kupona.”

124 Mungu ulisema

1. Mungu ulisema, Giza ilikoma; Twakushukuru! Twakusihi sote, Duniani mote Na kwa watu wote, Iwe nuru.    2. Yesu ulikuja, Ulituletea Nuru kuu; Macho kwa vipofu, Maisha kwa wafu; Twakushukuru.   3. Roho kiongozi, Roho wa mapenzi Tia nuru; Mwovu hata sasa Watu huwatosa, Tunakwomba hasa, Iwe nuru.   4. Mungu wa utatu Mwanga wao watu, Tuwe huru; Twende kote-kote Wafundishwe wote, Duniani mote, Iwe nuru.

125 Ati twonane Mtoni?

1. Ati twonane mtoni? Maji mazuri ya Mbingu; Yanatokea mwangani, Penye kiti cha Mungu. Naam, twonane mtoni! Watakatifu, kwenu ni mtoni! Tutakutanika mtoni Penye kiti cha Mungu.    2. Tukitembea mtoni Na Yesu mchunga wetu Daima tu ibadani Usoni pake kwetu.   3. Kwang’ara sana mtoni Cha Mwokozi ni kioo, Milele hatuachani, Tumsifu kwa nyimbo.   4. Si mbali sana mtoni, Karibu tutawasili, Mara huwa furahani Na amani ya kweli.

126 Ni mji mzuri

1. Ni mji mzuri, Mbali sana; Watu wanawiri Kama jua; Waimba kwa tamu, Tuna wema hakimu: Sifa na idumu, Kwake Bwana.    2. Ni mji mzuri Twende sote! Una na fahari Msikawe! Raha tutaona, Dhambi hapana tena; Hatutaachana Siku zote.   3. Ni mji mzuri; Macho yote Huko wanawiri Kama pete; Baba tutamwona, Tukifanywa tu wana; Tumo kupendana Naye sote.    4. Ni mji mzuri; Tusipotee Na tuwe hodari, Tuupate! Tufunze, tutume Kwa taji na ufalme: Sifa na zivume Siku zote.

127 Bwana Yesu atakuja

1. Bwana Yesu atakuja, Vumilia! Omba, ukiwa na haja, Vumilia! Mbingunu Mungu aliko, Mwamini Mwokozi wako, Nawe utafika huko, Vumilia!    2. Ikikucheka dunia, Vumilia! Mwovu atakuvizia, Vumilia! Hataweza kukushinda, Bwana Yesu akulinda, Roho yako, akupenda, Vumilia!   3. Na ukiwa hatarini, Vumilia! Dhiki nyingi duniani, Vumilia! Vyatupasa kuyakuta, Majaribu na matata, Na Bwana hakutuficha; Vumilia!   4. Adui wakikutana, Vumilia! Na ndugu wakikukana, Vumilia! Zote, zote zitakwisha, Nguvu zote za kutisha Mungu chini atashusha; Vumilia!    5. Moyoni una majonzi, Vumilia! Ndiyo bonde-ya-machozi, Vumilia! Hima tutaandamana, Kwetu Mbinguni na Bwana Tena hatutaachana; Vumilia!

128 Mmoja apita wote

1. Mmoja apita wote, Atupenda; Zaidi ya ndugu wote, Atupenda; Rafiki wa duniani, Wote hatuwaamini; Yesu kwa kila zamani, Atupenda.    2. Kumjua ni uzima, Atupenda; Jinsi ajaavyo wema Atupenda; Yeye ametununua Kwa damu aliyomwaga, Dhambini kutuokoa, Atupenda.   3. Sasa tunaye rafiki, Atupenda; Hupenda kutubariki; Atupenda; Twapenda kumsikia, Atwita kukaribia, Nasi tutamwamania, Atupenda.   4. Husamehe Dhambi zetu, Atupenda; Hushinda adui zetu, Atupenda; Anatwonea huruma, Hatupati ila mema, Anatwongoza salama, Atupenda. 

129 Karibu na wewe

1. Karibu na wewe, Mungu wangu Karibu zaidi, Bwana wangu Siku zote niwe Karibu na wewe, Karibu zaidi Mungu wangu.   2. Mimi nasafiri Duniani, Pa kupumzika Sipaoni, Nilalapo niwe Karibu na wewe, Karibu zaidi Mungu wangu.   3. Na kwa nguvu zangu Nikusifu; Mwamba, uwe maji Ya wokovu; Mashakani niwe Karibu na wewe; Karibu zaidi Mungu wangu.   4. Na nyumbani mwa juu, Baba yangu, Zikikoma hapa Siku zangu, Kwa furaha niwe Pamoja na wewe, Karibu kabisa Mungu wangu.

130 Niongoze, Bwana Mungu

1. Niongoze, Bwana Mungu, Ni msafiri chini; Ni mnyonge, nguvu sina: Nishike mkononi; U mkate wa Mbinguni, nilishe siku zote.    2. Kijito cha maji mema, Kitokacho mwambani, Nguzo yako, moto, wingu, Yaongoza jangwani; Niokoe mwenye nguvu; Nguvu zangu na ngao.   3. Nikikaribia kufa, Sichi neno lolote, Wewe kifo umeshinda Zinawe nguvu zote, Tutaimba sifa zako, Kwako juu milele.

131 Piga sana vita vyema

1. Piga sana vita vyema Kwa ushujaa daima, Yesu ndiye nguvu zako, Yesu ndiye kweli yako.   2. Kaza mwendo, ushindane Angaza macho, umwone Yesu ndiye njia yako, Naye ndiye tuzo lako.   3. Tupa kizito, simama, Tazama mbele, si nyuma; Ni yeye uzima wako, Naye ni kipendo chako.   4. Tangamka, uamini Akushika mikononi Hageuki, akupenda, Kuwa naye una pia.

132 Sauti sikilizeni

1. Sauti sikilizeni Za waimbao juu, “Aleluya, Aleluya, Aleluya, mkuu!” Wako makundi-makundi Kama nyota wang’ara, Kwa makuti ya mitende, Na meupe wamevaa.    2. Wazazi na manabii Wafanyaji wa njia; Mashahidi, waandishi, Nao wafalme pia! Mabikira kina-mama, Wajane wa kusali, Waimba wakikutana “Msifunu Imanweli”.   3. Watu toka huzunini Wameosha na nguo, Ni kwa damu yake Yesu; Maonjo, mbali nao! Walitekwa, walikatwa Hata kwa misumeno, Kwao kifo na shetani Walishindiwa mno.   4. Mungu mumo mwake Mungu, Nuru mumu mwa nuru, Kwa kufungamana mwako Tutaishi mahuru; Tujalize, Imanweli, Kujaa kwako wewe Mungu Baba, Mungu Mwana, Mungu Roho, tunawe.

133 Ni wako Mungu

1. Ni wako Mungu! Ni furaha kwangu, Ni raha kumjua mwokozi wangu.    Aleluya enzi ndako; Aleluya,Amin. Aleluya,enzi ndako; Rejea Yesu.    2. Mwana wa Mungu Ndiye fungu langu, Na moyo hufurahi kwa Yesu wangu.   3. Raha ya kweli Ina jina hili, Na aliyeshika,ana Mbingu kweli.   4. Nimeingia Mapendano haya, Nimepata uzima na Mbingu pia.   5. Nilipo chini, Ni mwako kazini Hata nije kwako uliko Mbinguni.

134 Juu yake langu shaka

1. Juu yake langu shaka, Yesu namuwekea, Nami sitafedheheka Nikimtegemea.    Natumai, natumai, Nnatumai kwake tu; Natumai, natumai, Natumai kwake tu.    2. Juu yake, dhambi zangu; Aniosha kwa damu; Nionekane kwa Mungu, Nisiye na laumu.   3. Juu yake yangu hofu; Kwake nimetulia; Sipotei kwa upofu Njia aning’azia.   4. Juu yake raha yangu; Humuangalia tu; Mwenye kila ulimwengu, Aniruzuku na huu.   5. Juu yake, moyo wangu; Hali yangu na mali; Mimi wake, Yeye wangu, Twapasana kamili.

135 Mapenzi ya milele

1. Mapenzi ya milele Ndiyo yanipendezayo; Yalinipenda mbele, Sina fahamu nayo; Sasa amani yake Tele rohoni mwangu, Ni mimi kwa kuwa wake, Na yeye kuwa wangu, Ni mimi kuwa wake, Na yeye kuwa wangu   2. Mbingu zinang’ara juu, Na nchi nayo vivyo; Macho ya dunia tu Hayajaona hivyo; Nyuni huimba sana, Maua yana rangi, Ni kumjua Bwana Na pendo zake nyingi, Ni kumjua Bwana Na pendo zake nyingi,   3. Mambo mengi maovu Nayo yenye kutisha, Sasa hayana nguvu, Si yenye kututisha; Ni mkononi mwake, Nalindwa salamani Ninajua ni wake, Ni wake mapenzini. Ninajua ni wake, Ni wake mapenzini.   4. Wake hata milele, Si kutengana tena; Hunipa raha tele Moyoni mwangu, Bwana; Hiyo nchi na Mbingu Zitatoweka zile, Ni wake, Yeye wangu, Milele na milele. Ni wake, Yeye wangu, Milele na milele.

136 Msifuni, Yesu ndiye mkombozi

1. Msifuni ,Yesu ndiye mkombozi; Imbeni ya pendo zake kuu, Sujuduni,malaika mlioko, Jina lake liwe na sifa kuu. Kama vile mchunga uchungavyo Vivyo sisi kutwa atachunga. Msifuni mlio wake watoto Msifuni aliye mchunga.    2. Msifuni,Yesu ndiye mkombozi; Akateswa tupate ongoka; Ndiye Mwamba,Dhamana ya kuokoka; Sujuduni kwake muangikwa, Yesu aliyeudhiwa na hamu Kwa pendo za baba yake Mungu. Aliyefyolewa na kusulubiwa. Msifuni ndilo letu fungu.   3. Msifuni,Yesu ndiye Mkombozi; Shindukeni,enyi malango juu; Bwana Yesu tangu milele Mwokozi, Mvikeni taji, ni yake tu. Atakuja kuitawala nchi, Yesu,Mwombezi wetu wa Mungu. Msifuni, ni mfalme wa salama; Ndiye kweli mwana wake Mungu.

137 Yesu mponya

1. Yesu ndiye mganga wetu Aponya wagonjwa wote; Mganga wetu ni Yesu, Aponyaye hasira.    Tumsifu huyo Yesu Tumsifu milele, Kwani Mponya mtakata Mwokozi wa wanyonge   2. Mganga wetu ni Yesu Huondoa matusi; Mganga wetu ni Yesu, Mwenye kuponya choyo.   3. Mganga wetu ni Yesu Huponya wivu wetu; Yesu ndiye aponyae Kelele za nyumbani.   4. Mganga wetu ni Yesu Mponya wa tamaa mbaya; Mganga wetu ni Yesu Uasherati hufuta   5. Mganga wetu ni Yesu Aponya kiu cha pombe, Mganga wetu ni Yesu Kila dhambi uponya

138 Tukutendereza Yesu (Luganda)

1. Yesu, Mulokozi wange: Lero nze wuwo wenka; Omusaigwo gunazi’za Yesu Mwana gwendiga.   Tukutendereza, Yesu, Yesu Mwana gwendiga; Omusaigwo gunazi’za; Nkwebaza, Mulokozi.   2. Eda nafuba bufubi Okufuna, emirembe; Lero maliride dala Okweyabiza Yesu.   3. Nababuliranga bantu Obulokozi bwona, Obutali bwa kitundu Obulamba obwobuwa   4. Nategezanga ebya Yesu Nobuvumunesitya; Eyanziya mu busibe Nokuwonya eyamponya.   5. Nebaza eyanunula nze; Eyamponya wa kisa! Yesu ankuma Ansanyusaera, Bulijo yebazibwe.

139 Nuru ya rohoni

1. Nuru ya rohoni ni Bwana Yesu. Nakuomba sana niangazishe; ukanitazame kwa huruma tu,   ukanitulize mimi maskini.   2. Futa dhambi zangu kwa damu yako. Hasira ya Mungu iniondoke. Machubuko yako, hata mateso,   niyawaze vema rohoni mwangu.   3. Nakutumaini peke yako tu, niwe mtumwa wako pote nilipo utanikubali sina mashaka!   Nitakushukuru pasipo mwisho.

140 Mahali ni pazuri

1. Mahali ni pazuri, ndugu wanapokaa, wakipatana vema, na wakipendana.   2. Kama umande mzuri, unyweshavyo shamba, vivyo na Mungu wetu, hubariki ndugu.   3. Upendano hujenga, boma zuri kwao, wakae na amani, waliookakoka.    4. Na ulimwengu wote, watiwa nuruni, halafu kundi moja, na mchunga mmoja tu. 

141 Pana jito, lina maji mazuri

1. Pana jito, lina maji Mazuri, Yaenda ulimwenguni. Lametameta nalo Linang’aa. Walijua jito hilo?   Ninakuita nawe njoo! Utafute jito hilo! Maji yake yapoza Moyo. Nawe yateke unywe.   2. wanywao maji haya wafurahi, waimba kwa shangwe kubwa. Makosa na shida Yanaondoshwa, Wote waoshwa na Bwana. Ninakuita nawe njoo …   3. Jito hilo latoa maji mengi, matamu yapendezayo. Yaponya wagonjwa, Yatia nguvu, Uchafu watakashika. Ninakuita nawe njoo …   4. maji ya jito hilo ni uzima unaotoka Kwa Yesu. Damu yake yenye kiasi kikuu Imemwagwa tusafike. Ninakuita nawe njoo …

142 Babangu kule mbiguni.

1. Babangu kule mbinguni, aliye juu pa malaika, aangalia njia zangu na kunilinda maisha.   2. Hata unywele kichwani hauanguki ovyo tu na siri zote za moyoni zajulikana kwa Baba.   3. Zamani nisipojua, amekwisha kuandika mkononi mwake jina langu, ndio upedo wake mkuu.   4. Ee Baba yangu u mwema, nami nataka kufanya kama malaika wafanyavyo mbinguni kwako milele!.

143 Nchi nzuri yametameta

1. Nchi nzuri yametameta, Huonekana kule mbali, Naye Yesu hutuongoza. Tukafike na sisi huko.   Sisi mbali, karibu, Tutaimba na sisi huko!   2. Kule tutawaona wengi Wapendwao na Yesu Bwana, Tutashirikiana nao Itakuwa furaha kubwa. Si mbali..   3. Tutamwona na Bwana Wetu, Yesu kristo mwokozi Wetu, Tutashangilia daima, Tuna hamu ya kwenda Kwetu. Si mbali..

144 Mbele ninaendelea

1. Mbele ninaendelea, ninazidi kutembea. Maombi uyasikie, Ee Bwana, unipandishe.   Ee, Bwana, uniinue, Kwa imani nisimame; Nipande milima yote, Ee Bwana, Unipandishe.   2. Sina tamani nikae, Mahali pa shaka, kamwe; Hapo wengi wanakaa, Kuendelea naomba.   3. Nisikae duniani, asumbuapo Shetani; Natazamia mbinguni, nitafika na amani.   4. Nataka nipandishwe juu, Zaidi yale mawingu. Nitaomba nifikishwe, Ee Bwana unipandishe.

145 Ndoa yetu nzima

1. Ndoa yetu nzima simika, Yesu! Usiku na mchana uwepo kwetu. Leo tuna raha, Wewe watupa. Ndoa yetu Bwana ndiwe Baraka!   2. Atoka kijana, ataka mchumba siku zinapita za kupimana. Leo twapatana pamoja kukaa Ndoa yetu…   3. Vyote hapa chini vinakaa muda, vyote vinaoza, tena vyachakaa. Pendo la duniani nalo huchakaa Ndoa yetu…   4. Kakaa kwetu Bwana, kutukagua, pendo letu sisi lisichakae: Hivi na tukae na baraka tu. Ndoa yetu…   5. Kana arusuni ulialikwa, walivyoishiwa ukaongeza, nasi shida zetu utazishinda. Ndoa yetu..

146 Neno la Mungu takata

1. Neno la Mungu takata Lililotoka mbinguni; Ambalo moto na panga Haziwezi kulishinda.   /: Twakushika siku zote Maishani na kufani . :/   2. Waliotutangulia Waliokutegemea, Wamekufia mashujaa; Nasi tulio watoto. Twakushika …   3. Neno la Mungu takata, Tukushuhudie nasi Kwa neno tamu na tendo Kunako wenzi au adui. Twakushika …

147 Tegemea mpaka kufa

  1. Tegemea mpaka kufa, Utapata wokovu. Bwana Yesu ni Mwokozi Yeye anakupenda. Uje kwake ‘sikawie’. Yeye akuokoa. Njoo upesi! Njoo upesi! Fika kwa Bwana Yesu.   2. Acha mambo ya dunia Yakuhangaishayo. Iko mali ya uzima Unaitiwaa hiyo. Mali hiyo ni uzima Utapewa na Bwana. Njoo upesi! …   3. Wakatae, waepuke Wanaokudanganya; Na wajinga, wakuponza, Wakupoteza wewe. Ila wewe ukatae Kuondoka kwa Yesu. Njoo upesi! …   4. Ukijua jambo hilo Usipolifuata Kosa hilo kubwa sana, Wapasiwa hukumu. Vumilia, jizuie Utapata uzima. Njoo upesi! …   5. Bwana Yesu amekwisha Kukutengenezea Kitu chema kwake Mungu, Ndiko unakokwenda. Kile kitu upendacho Kule utakipewa. Njoo upesi! …

148 Ondokeni! Tunaitwa

  1. Ondokeni! tunaitwa na walinzi wa juu mnarani Yerusalemu, amka wee! Ni usiku wa manane, yuaja Bwana wa arusi, wanawali wako wapi? Amkeni upesi! Kaziwasheni taa. Haleluya! Fuateni arusini kwenda kumpokea Bwana!   2. Sayuni anasikia, moyo waruka kwa furaha, yu macho anaondoka. Mponya wake anashuka mbinguni mwenye utukufu, aleta mwanga wa kweli, taji yake yaja na Mwana wa Mungu. Hosiana! Twafuata kwenye shangwe tukale karamu yake.   3. Waimbiwa nyimbo nzuri kwa misemo ya watu wote na ya malaika mbinguni. Tukifika mjini kwako kwenye milango ya malulu tutakuimbia nasi. Furaha kama hii haijasikiwa duniani. Nasi sasa tunaimba, tunakusifu, Ee Bwana.

149 Haya, Umati wa Yesu

  1. Haya, umati wa Yesu, Ulioungwa naye! Haya, enendeni hima Katika vita kubwa! Shetani tayari, Kupigana na sisi!   2. Tumfuate Yesu Kristo, Tumwamini yeye tu. Mwovu akituvizia Sisi hatuogopi. Majeshi ya mbingu Ni pamoja na sisi!   3. Tukikesha na kuomba Yesu anayotaka, Tukishika neno lake Na kumtegemea Kwa nguvu hizi tu Tutaweza kushinda!   4. Sasa haya wenzi wangu, Tumfuate Yesu tu! Siku za maisha yetu, Tuwe katika yeye. Tuache dunia Kuingia mbinguni!   5. Pale Mungu atawapa Taji walioshinda, Wapate urithi wao Nyumbani mwa milele. Hayani! Tuimbe, Tumsifu Bwana wetu!