Posts

Showing posts from April, 2022

30 Nilikuwa kondoo aliyepotea

1. Nilikuwa kondoo aliyepotea, Sikupenda zizi kamwe, ila kutembea Nilikuwa mwana asiyesikia, Sikupenda baba yangu wala kutulia.    2. Na mchunga mwema alinitafuta, Baba kwa mapenzi ndiye aliyenivuta; Karibu ya kufa, kwa kiu na kwa njaa, Waliniona mnyonge, waliniokoa.   3. Yesu ni mchunga, mwenziwe hapana, Aliosha taka zangu, dhambi nyingi sana; Kwa vidonda vyangu alitia dawa. Ndiye aliyenipata, na kwake nalindwa.   4. Nilikuwa kondoo aliyepotea Sasa nampenda Baba, na mchunga pia; Kwanza nilitanga na kukosa sana, Hivi nyumbani mwa Baba sipotei tena. 

31 Msingi imara

1. Msingi imara, enyi wa kweli, Umekwisha pigwa kwa neno hili; Aongeze lipi? Mnayo pia Kwa Yesu mliomkimbilia.    2. Wambiwapo vuka maji ya giza, Mito ya mashaka taipunguza; Takupa nawe, nikuwezeshe, Ipata kufaa, isikutishe!   3. Utakapopishwa ndani ya moto Nnguvu nitakupa, upate pato; Huteketezwi, ila taka zako, Na zitasalia dhahabu zako.   4. Hata zije mvi, walio wangu Hawaoni kwisha mapenzi yangu; Nazo zitakapowenea, ndipo Mabegani mwangu niwatwekapo.   5. Na mtu aliyenitegemea Kamwe kwa adui sitamtia; Nguvu za jehanam zijapotisha, Mtu wangu kamwe sitamuacha.

32 Yesu awakubali wakosa

1. Yesu awakubali, Wakosa, wahalifu, Wambieni wa mbali Habari ya wokovu.    Tangazeni kwa bidii, “Akubali wakosa!” Liwe neno dhahiri, “Akubali wakosa!”    2. Awakubali Bwana Neno lake amini Watu kila aina Waje kwake tengoni.   3. Mimi ni safi moyo Na mbele ya sharia, Aliye safi roho Kwake ilitimia.   4. Akubali wakosa; Nami anikubali; Alivyonitakasa Mbinguni niwasili.

33 Dhambi ikikulemea

1. Dhambi ikikulemea, Kwa Bwana rehema; Hivi sasa tegemea Neno la salama.    Tegemea, tegemea, akwita sasa. Ni Mwokozi, ni Mwokozi; amini sasa.    2. Yesu amemwaga damu Ya nyingi baraka; Nawe sasa oga mumu Zioshwamo taka.   3. Ni njia yeye hakika Hwongoza rahani; Usikawe kumshika, Uwe barakani.   4. Karibu nawe wingie Mwetu safarini, Twende tukamwamkie, Milele Mbinguni. 

34 Njoni! Wenye dhambi

1. Njoni! Njoni! Wenye dhambi, Njoni, msikawie; Yesu awangojea ndiye awapendaye; Ajuaye awezaye kuwaponya ni Yeye.    2. Ewe muhitaji uje; Anakukaribisha, Imani, kweli, na toba, Neema ya kutosha, Jua sana, kwake Bwana Bure utapata.   3. Njoni, mliolemewa Na dhambi ya Adamu; Mkingoja kujiponya Mtapotea mumu; Si wa haki, ni wakosa Waoshwao kwa damu.   4. Ikamtokea dhiki, Mle Gethisemani; Kisha alipoangikwa Akalia mtini; ” Imekwisha”, alitosha Dhabihu ya thamani.   5. Kristo aliye Mbinguni Hutuombea huko; Basi mtumai yeye; Kamwe mwingine hako Yesu pweke, Yesu pweke, Ndiye Mwokozi wako.   6. Wamsifu-sifu sana Mbinguni malaika; Wachanganya nyimbo zao Na waliookoka: Aleluya wataimba Waliooshwa taka. 

37.Waitwa, Mwovu, na Bwana

Waitwa, mwovu, na Bwana Umwendee hima sana, Usafiwe dhambi zako, Humwoni ni mwema kwako? Unaitwa! Itika tu! Umwendee Bwana Yesu! Sifiche makosa yako, Uungame dhambi zako! Kristo tu umuamini, Ndiyo njia ua Mbinguni. Alilipa damu yake Ili kukukweza kwake; Alikufa yeye Bwana, Mimi nawe tuwe wema. Ukifanywa kuwa mwema Mwishoni utasimama, Utaingia rahani Na wapenzi wa zamani. Ni mwanga tu, nchi ile; Uovu hauko kule, Kwamba wataka ufike Sharti huku uosheke.

35 Twende kwake

1. Twende kwake, twende kwake, kwake Yesu sasa, Sasa twende kwake, kwake Yesu sasa!    2. Akwokoe. akwokoe, Bwana Yesu sasa! Sasa akwokoe, Bwana Yesu, sasa!   3. Msadiki, msadiki, Bwana Yesu sasa, Sasa msadiki, Bwana Yesu sasa!   4. Anaweza, anaweza, Bwana Yesu sasa, Sasa anaweza, Bwana Yesu sasa!   5. Anapenda, anapenda, Bwana Yesu, sasa, Sasa anapenda, Bwana Yesu sasa!   6. Njoo hima, njoo hima, kwake Yesu sasa, Sasa njoo hima, kwake Yesu, sasa! 

36 Anisikiaye aliye yote

1. Anisikiaye, aliye yote; Sasa litangae, wajue wote, Duniani kote neno wapate, Atakaye na aje!    Ni “Atakaye”, ni “atakaye”, Pwani hata bara, na litangae; Ni Baba Mpenzi alinganaye Atakaye na aje.    2. Anijiliaye, Yesu asema, Asikawe, aje hima mapema; Ndimi njia, kweli, ndimi uzima; Atakaye na aje!   3. Atakaye aje, ndivyo ahadi; Atakaye hiyo, haitarudi! Atakaye lake, ni la abadi! Atakaye na aje. 

38 Twende kwa Yesu

1. Twende kwa Yesu mimi nawe, Njia atwonya tuijue Imo Chuoni; na Mwenyewe, Hapa asema, Njoo!   Na furaha tutaiona, Mioyo ikitakata sana, Kwako, Mwokozi, kuonana, Na milele kukaa.   2. ”Wana na waje”, atwambia, Furahini mkisikia, Ndiye mfalme wetu pia, Na tumtii, Njoo.   3. Wangojeani? Leo yupo; Sikiza sana asemapo; Huruma zake zikiwapo, Ewe kijana, Njoo. 

39 Mwenye dhambi huna raha

1. Mwenye dhambi huna raha, Sikiza nakusihi, Utapata msamaha Kwake Yesu Mwokozi! Njoo hima, njoo hima, Naye atafurahi.    2. Yesu anakwita sana Naye yuko Mbinguni; Hofu ya kifo hapana Kwake ukiamini. Njoo hima, njoo hima, Utapata amani.   3. Hatakwita siku zote; Ni ya sasa nafasi. Lete na uchafu wote, Kukawa haipasi. Njoo hima, njoo hima, Ni wokovu halisi.   4. Uzima uko kwa Bwana Twae uzima hasa Bure unapatikana, Wokovu twae sasa! Njoo hima, njoo hima, Twae utakatifu. 

41 Yesu aliniita, “Njoo”

1. Yesu aliniita, “njoo, Raha iko kwangu, Kichwa chako ukilaze Kifuani mwangu.” Nilikwenda kwake mara, Sana nilichoka; Nikapata kwake raha, Na furaha tena.    2. Yesu aliniita, “njoo, Kwangu kuna maji, Maji ya uzima, bure, Unywe uwe hai, ” Nilikwenda kwake mara Na maji nikanywa: Naishi kwake, na kiu Kamwe sina tena.   3. Yesu aliniita, “njoo, Dunia ni giza, Ukinitazama nuru Takung’arizia.” Nilikwenda kwake mara Yeye jua langu, Ni kila wakati mwanga Safarini mwangu. 

40 Nasikia kuitwa

1. Nasikia kwitwa Na sauti yako Nikasafiwe kwa damu Ya kwangikwa kwako. Nimesogea Mtini pako, Unisafi kwa damu ya kwangikwa kwako.    2. Ni mnuonge kweli, Umenipa nguvu, Ulivyonisafi taka, Ni utimilivu.   3. Yesu hunijuvya; Mapenzi, imani; Tumai, amani, radhi, Hapa na Mbinguni.   4. Huipa imara, Kazi yake, ndani: Huongezeka neema, Ashindwe Shetani.   5. Huishuhudia, Myoyo ya imani Ya kuzipata ahadi, Wakimuamini.   6. Napata wokovu, Wema na neema; kwako Bwana nina nguvu Na haki daima. 

42 Kivulini mwa Yesu

1. Kivulini mwa Yesu kuna Kituo: Kituo mbali na hamu, kituo kilicho tamu. Kivulini mwa Yesu kuna kituo; kivulini mwa Yesu kuna kituo; Raha tu, mle; amani tupu, Furaha tele; kivulini mwa Yesu Raha tu, mle; amani tupu, Furaha tele; kivulini mwa Yesu.  2. Kivulini mwa Yesu nina amani Iliyopita fahamu, tena itakayodumu.   3. Kivulini mwa Yesu, nina furaha; Furaha yenye fahari, ya kueneza habari. 

43 Yesu akwita

1. Yesu akwita, chanena Chuo: Uje leo, uje leo; Kwani kusita? Akwita, Njoo; Unatanga upeo.    Hwita leo, hwita leo. Yesu akwita kwa upole akwita leo.    2. Waliochoka, wapumzike, Hwita leo, hwita leo: Wenye mizigo, wakamtweke, wapate mapumuo.   3. Anakungoja, uliye yote, Uje leo, uje leo; Uliyekosa usijifiche: Woshwe, uvikwe nguo.   4. Yesu asihi wakawiao, Waje leo, waje leo. Watafurahi waaminio; Usije kwani? Njoo. 

44 Kukawa na giza dunia yote

1. Kukawa na giza dunia yote, Ni Mwanga wa ulimwengu, Ikaisha ulipokuja yote, Ni mwanga wa ulimwengu.    Jua, Yesu hana mwenziwe! Nalipofuka kama wewe: Nakuombea umwone nawe, Ni mwanga wa ulimwengu.    2. Hatuna giza tudumuo mwake, Ni mwanga wa ulimwengu; Tumwandamiapo nyayoni mwake Ni mwanga wa ulimwengu.   3. Enyi wa gizani wenye kutanga! Ni mwanga wa ulimwengu, Kaulekeeni, mpate lenga; Ni mwanga wa ulimwengu.   4. Tutamwona Mwokozi juu ya mbingu Ni mwanga wa ulimwengu: Ni nuru za mbingu kondoo wa Mungu Ni mwanga wa ulimwengu. 

45 Mtazame Huyo aliyeangikwa juu

1. Mtazame Huyo! Aliyeangikwa juu Hivi sasa upate ishi. Mwenye – dhambi dhaifu, mtazame tu Wala usifanye tashwishi.    Tazama! Tazama! Tazama uishi! Mtazame huyo aliyeangikwa juu Hivi sasa upate ishi.    2. Kama mwana kondoo hakuondoa dhambi, Na makosa yako maovu! Kama deni zetu zote hakulipa Mbona imemwagika damu?   3. Si kutubu na sala ikomboayo, Ila damu ndiyo salama; Na aliyeimwaga aweza, sasa, Dhambi zako kukufutia.   4. Usiwe na shaka, Mungu amesema, Hakuna alilolisaza; Hapo alipokuja alitimiza Kazi zote alizoanza.   5. Basi twae uzima, kwa kufurahi Upokee kwa Bwana, sasa; Ujijue hakika kwake kuishi Yesu aishiye kabisa. 

46 Twae wangu uzima

1. Twae wangu uzima, Sadaka ya daima; Twae saa na siku, Zikutukuze huku.    2. Twae mikono nayo Ifanye upendavyo, Twae yangu miguu Kwa wongozi wako tu.   3. Twae sauti yangu, Niimbe kwa Mungu tu; Itwae na midomo, Ijae neno lako.   4. Twae dhahabu pia, Na yote ya dunia; Twae yangu hekima, Upendavyo tumia.   5. Nia itwae, Mungu, Haitakuwa yangu; Twae moyo; ni wako, Uwe makazi yako.   6. Twae mapenzi yangu, Sifa za moyo wangu; Twae kabisa nafsi Niwe wako halisi. 

47 Ni wako wewe

1. Ni wako wewe, nimekujua, Na umeniambia; Lakini Bwana, nataka kwako nizidi kusongea.    Bwana vuta, vuta, nije nisongee, Sana, kwako mtini. Bwana vuta, vuta, nije nisongee, Pia damu ya thamani.    2. Niweke sasa nikatumike Kwa nguvu za neema; Uyapendayo nami nipende, Nizidi kukwandama.   3. Nina furaha tele kila saa Nizungumzavyo kwako, Nikuombapo nami napata kujua nia yako.   4. Mapenzi yako hayapimiki, Ila ng’ambo ya liko. Anasa pia sitazijua, Bila kufika kwako. 

48 Naweka dhambi zangu

1. Naweka dhambi zangu Juu yake Bwana Kuziondoa, kwangu Hulemea sana; Na uaili wangu Ameuondoa; Dawa yangu ni damu, Kwa hiyo napoa.    2. Na uhitaji wangu Nitamjuvisha Kwa upungufu wangu Yeye anatosha; Majonzi yangu yote Na mizigo yangu, Atachukua vyote Yesu Bwana wangu.   3. Na roho yangu nayo, Imechoka sana; Namletea hiyo Ilindwe na Bwana; Ni jema jina lake, Nalo lapendeza, Imanweli na kwake tutalitukuza.   4. Natamani daima Niwe kama Bwana, Mpole, tena mwema, Wa mapenzi sana; Zaidi natamani Kwenda kwake juu, Nikaone mbinguni Enzi yake kuu. 

49 Nitwae hivi nilivyo

1. Nitwae hivi nilivyo, Umemwaga damu yako, Nawe ulivyoniita, Bwana Yesu,naja,naja.   2. Hivi nilivyo;si langu Kujiosha roho yangu; Nisamehe dhambi zangu, Bwana Yesu,naja,naja.   3. Hivi nilivyo; sioni Kamwe furaha moyoni; Daima ni mashakani, Bwana Yesu,naja,naja.   4. Hivi nilivyo kipofu, maskini na mpungufu; Wewe u mtimilifu; Bwana Yesu,naja,naja.   5. Nawe hivi utanitwaa; Nisithubutu kukawa, Na wewe hutanikataa, Bwana Yesu,naja,naja.   6. Hivi nilivyo;mapenzi Yamenipa njia wazi; Hali na mali sisazi, Bwana Yesu,naja,naja. 

50 Yesu nakupenda, U mali yangu

1. Yesu nakupenda, U mali yangu, Anasa za dhambi sitaki kwangu; Na Mwokozi aliyeniokoa, Sasa nakupenda, kuzidi pia.    2. Moyo umejaa mapenzi tele Kwa vile ulivyonipenda mbele, Uhai wako ukanitolea Sasa nakupenda, kuzidi pia.   3. Ulipoangikwa Msalabani Tusamehewe tulio dhambini; Taji ya miiba uliyoivaa, Sasa nakupenda, kuzidi pia.   4. Niwapo hai, niwapo maiti, Kupendana nawe kamwe siachi; Hari za kifo zikinienea, Sasa nakupenda, kuzidi pia.   5. Mawanda mazuri, na masikani Niyatazamapo huko Mbinguni, Tasema na taji nitakayovaa Sasa nakupenda, kuzidi pia. 

51 Mungu twatoa shukrani

Mungu twatoa shukrani, Kwa kutulinda usikuni, Na kutuangalia mchana, Kutuongoza kila mara.

52 Yote namtolea Yesu

1. Yote namtolea Yesu Nampa moyo wote, Nitampenda siku zote, Namwandama kila saa.    Yote kwa Yesu, Yote kwa Yesu, Yote kwako, Ee mwokozi, Natoa sasa.    2. Yote namtolea Yesu, Nainamia pake; Nimeacha na anasa, Kwako Yesu nipokee,    3. Yote namtolea Yesu, Nifanye niwe wako; Nipe Roho yako, Bwana, Anilinde daima,    4. Yote namtolea Yesu, Nami naona sasa; Furaha ya ukombozi, Nasifu jina lake, 

53 Wewe umechoka sana

1. Wewe umechoka sana? Wataka raha? Kwake Yesu utapata furaha.    2. Alama anazo yeye? Sasa! makovu ya mikono, na miguu, Na mbavu.   3. Nacho kimivukwa taji Kichwa cha huba? Alivikwa taji kweli miiba.   4. Huku nikimfuata nipate nini? Maonjo nje na ndani amani.   5. Kwamba namwandama Bwana, Mwisho ni nini? Ni furaha na salama Mbinguni. 

54 Yesu nataka kutakaswa sana

1. Yesu nataka kutakaswa sana, Nataka moyo uwe enzi yako. Ukiangushe kilichoinuka Unioshe sasa niwe mweupe.    Mweupe tu, ndiyo mweupe, Ukiniosha nitakuwa safi.    2. Bwaba Yesu, unitazame sasa, Unifanye niwe dhabihu hai; Najitoa kwako, na moyo wote; Unioshe sasa niwe mweupe.   3. Bwana kwa hiyo nakuomba sana, Nakungojea miguuni pako, Naomba unioshe damuni tu, Unioshe sasa niwe mweupe.   4. Bwana nidumu kukungojea, Niumbie moyo safi, Ee Mungu, Wanaokujia hutupi kamwe, Unioshe sasa niwe mweupe. 

55 Nipe moyo wenye sifa

1. Nipe moyo wenye sifa Sio wa utumwa; Moyo ulionyunyizwa Damu ya thamani.    2. Moyo msikizi, moyo Wa kunyenyekea, Moyo utawaliwao Na Mwokozi pia.   3. Mwenye kutubu, mnyonge, Sadiki, amini; Kamwe, kamwe asitengwe Akaaye ndani.   4. Mpya, mwema na mawazo Mwingi wa mapenzi Nawe uwe kielelezo Moyo wa Mwokozi.   5. Ni uule moyo wako; Moyo wa huruma Yesu, natamani kwako Kukujua vyema.   6. Na ya midomo matunda Yako, nipe nami; Amani isiyokoma Iwe yangu mimi.   7. Nitie yako tabia, Inishukie juu; Jina lako nipe pia, Ndilo la upendo.   8. Ni wa baba utukufu; Mwana atukuke; Na roho Mtakatifu U utatu pweke. 

56 Ni sikukuu siku ile

1. Ni siku kuu siku ile Ya kumkiri Mwokozi! Moyo umejaa tele, Kunyamaza hauwezi. Siku kuu! Siku kuu! Ya kuoshwa dambi zangu kuu! Hukesha na kuomba tu, Ananiongoza miguu. Siku kuu! siku kuu! Ya kuoshwa dhambi zangu kuu.    2. Tumekwisha kupatana Mimi wake, yeye wangu, Na sasa nitamwandama, Nikiri neno la Mungu.   3. Moyo tulia kwa Bwana Kiini cha raha yako, Huna njia mbili tena; Yesu ndiye njia yako.   4. Nadhiri yangu ya mbele Nitaiweka daima, Hata ije siku ile, Ya kwonana kwa salama 

57 Naendea msalaba

1. Naendea Msalaba, Ni mnyonge na mpofu, Yapitayo naacha, Nipone Msalabani.    Nakutumaini tu, Ewe Mwana wa Mungu; Nainamia kwako; Niponye, mponya wangu.    2. Nakulilia sana: Nalemewa na dhambi; Pole Yesu asema; “Nitazifuta zote”.   3. Natoa vyote kwako, Nafasi nazo nguvu, Roho yangu na mwili, Viwe vyako milele.   4. Kwa damu yake sasa, Nimegeuka roho, Nikaziacha tama Nimfuate Yesu tu.   5. Yesu yuaja tena! Nimepevuka kwake, Kila chembe kamili; Msifuni yeye mponya! 

58 Mwamba mwenye imara

1. Mwamba wenye imara Kwako nitajificha! Maji hayo na damu Yaliyotoka humu, Hunisafi na dhambi, Hunifanya mshindi.   2. Kwa kazi zote pia , Sitimizi sharia. Nijapofanya bidii, Nikilia nakudhii, Hayaishi makosa; Ndiwe wa kuokoa.   3. Sina cha mkononi, Naja Msalabani; Nili tupu, nivike; Ni mnyonge, nishike; Nili mchafu naja, Nioshe nisijafa.   4. Nikungojapo chini, Nakwenda kaburini; Nipaapo Mbinguni, Na kukwona enzini: Roho yangu na iwe Rahani mwako wewe. 

59 Peleleza ndani yangu

1. Peleleza ndani yangu, Iwe safi nia, Kwangu kama kwako Mungu, Idhihiri pia.    2. Peleleza moyo wangu Uunifunulie, Yaliyomo ndani yangu Nami niyajue.   3. Kwanza washe zako tambi, Kumefunga giza; Nijue ambavyo dhambi Ni la kuchukiza.   4. Peleleza na mawazo Ni mbegu za mambo, Asili ya machukizo, Maumbuo – umbo.   5. Zidi kuyapeleleza Katikati yangu Hata wishe nifundisha Udhaifu wangu.   6. Hapo nikikwinamia Mbele zako, Mungu, Hakika nitakujua U mpenzi wangu. 

60 Waponyeni watu

1. Waponyeni watu wamo kifoni, Watoeni walio shimoni; Na aangukaye mumzuie; Ya Bwana Yesu wahubirini.    Walio kifoni waokoeni, Mwokozi yuko, wahubirini.    2. Wajapokawia anangojea, Awasubiri waje tobani; Msiwadharau, muwaonyeni; Huwasamehe; wakiamini.   3. Myoyoni mwa ndani, yule shetani Ameyaseta mawazo yao; Lakini kwa Bwana huwa mazima, Tukiwavuta kwa pole hao.   4. Kawaokoeni, wale njiani, Mutimize mapenzi ya Bwana; Na kwa nguvu zake warudi kwake, Kwa subira waonyeni sana. 

61 Tumesikia mbiu

1. Tumesikia mbiu: Yesu lo! aponya, Utangazeni kote, Yesu, lo! aponya. Tiini amri hiyo; Nchini na baharini, Enezeni mbiu hii; Yesu , lo! Aponya.    2. Imbeni na vitani: Yesu, lo! Aponya; Kwa nguvu ya kombozi, Yesu, lo! Aponya. Imbeni wenye shida, Unapoumwa moyo. Na kaburini imba; Yesu, lo! Aponya.   3. Mawimbini uenee; Yesu, lo! Aponya; Wenye dhambi jueni; Yesu, lo! Aponya. Visiwa na viimbe, Vilindi itikeni, Na nchi shangilieni; Yesu, lo! Aponya.   4. Upepo utangaze; Yesu, lo! Aponya; Mataifa yashangaaa; Yesu lo! Aponya. Milimani, bondeni, Sauti isikike Ya wimbo wa ushindi; Yesu, lo! Aponya. 

62 Bwana wa mabwana

1. Bwana wa mabwana, Mwenye nguvu sana Twakusihi: Neno la milele Na liende mbele, Waongoke tele Kwa Mwokozi.    2. Tunaowaona Wanavyopatana, Kulipinga, Hawataliweza Neno, kulitweza: Huwaje! Kucheza: Na upanga?   3. Heri wajitunze Ili wapatane, Na Mwokozi; Watafute sana, Wapate kuona, Yesu kuwa Bwana, Mkombozi.   4. Mungu awaita Wasije kukuta Pigo lake; Hakuona vyema Wakose uzima, Awape rehema, Waokoke.   5. Mwenye utukufu Tunamshukuru Yeye pweke! Nasifiwe sana, Baba, naye Mwana, Na wa tatu tena Roho yake. 

63 Ndugu wa kirohoni

1. Ndugu wa kirohoni Mliokombolewa, Tafakarini sana Yatupasayo.    Wapenzi wake Yesu Tuliokombolewa Tujitoe kabisa Wengi waponywe.    2. Siku itatimia Tutakapoulizwa Wale wa nyumba zetu Na majirani   3. Tujitoeni, ndugu, Tukahubiri Injili. Atutumie Roho kuponya wengi.   4. Wasiokombolewa Ni wengi vijijini, Wataokolewaje Tukiogopa?   5. Bwana alijitoa Akapotewa mengi, Ili atuokoe, Tusiwe waoga.   6. Aliyetununua, Kwa kuimwaga damu, Angalieni sana Msimwepuke. 

64 Ujaribiwapo, sifanye dhambi

1. Ujaribiwapo, sifanye dhambi, Bali uzishinde, kwa Yesu kutii. Fuliza kiume ushinde tamaa; Yesu ni Mwokozi, hukuokoa. Umwombapo yu papo Akuongeze nguvu, Atakusaidia; Yesu atakufaa.  2. Wepushe waovu, matusi dharau; Heshima la Mungu, kamwe sisahau; Fanya uhodari, uwe mpole, Atakuokoa hata milele.   3. Avumiliaye hupewa taji; Tujaposumbuka tu washindaji, Na mwokozi wetu hutuwezesha Tusiwe kushindwa kama twakesha. 

65 Safari

1. Katika safari yetu Kwenda Mbinguni Tusiishe siku zetu Usingizini.    Ng’oani! Tujifungeni, Twende zetu juu! Kristo ndiye kiongozi; Tusihofu tu.    2. Atwekwe badala yetu, Mwenyewe Bwana; Yesu kiongozi wetu Atapokea.   3. Kisimani, maji tele, Maji mazima! Maji hayo, Ya milele Yana neema.   4. Njiani miiba mingi, Yatuumiza; Hofu na hatari nyingi, Sana zakaza.   5. Kweli, njia ya Mbinguni Ni ya mashaka; Tuwe na Yesu njiani, Mara hufika. 

66 Po pote mashamba yajaa

1. Po pote mashamba yajaa, Tele nafaka pevu, Po pote yang’aa meupe Bondeni na nyandani. Mwenye mavuno, wasihi Upeleke wavuni, Wakusanye mazao, Hata kazi iishe.    2. Wapeleke uchaoni, Waende na jotoni, Mpaka jua lishukapo Wakusanye ko kote.   3. Watenda kazi wa Bwana, Mlete sasa mazao, Na jioni ingieni Kwake na furaha kuu. 

67 Bwana uliyewaita

1. Bwana uliyewaita Watakatifu wako, Wawe mitume, wachunga, Walishe kundi lako; wanyonge na wenye hofu Wakawa mashujaa, Na wapole wa kunena Wasiwe kunyamaa.    2. Hata leo wawataka Watakatifu wako, Nawe wauliza tena Ni nani aliyeko Atakaye nimtume Afundishe vijana? “Ni tayari, Bwana wangu, Nitume mimi Bwana.”   3. Nitume na mimi, Bwana Kama ulivyotumwa, Habari ya msamaha Na dhambi kutubiwa, Niwahubiri wakosa, Na waliopotea, Wokovu u wake Bwana, Aliyewafilia.   4. Astahiliye hapana Kutamka habari, Lakini wewe waweza Kutufanya tayari. Neno lako tulijue, Tupe na roho yako, Hayatakuwa ya bure, Haya maneno yako. 

68 Mungu msaada wetu

1. Mungu msaada wetu Tangu myaka yote, Ndiwe tumaini letu La zamani zote.    2. Kivuli cha kiti chako Ndiyo ngome yetu. Watosha mkono wako Ni ulinzi wetu.   3. Kwanza havijakuwako Nchi na milima, Ndiwe Mungu; chini yako Twakaa salama.   4. Na myaka elfu ni kama Siku moja kwako; Utanilinda daima Tu wenyeji wako.   5. Binadamu huondoka, Mwisho hana kitu; Kama ndoto hutoweka Ndivyo hali yetu.   6. Ila wewe Mungu wetu Ndiwe wa kudumu; Ndiwe bora, ngome yetu Twakaa dawamu. 

69 Twendeni askari

  1. Twendeni askari, watu wa Mungu; Yesu yuko mbele, tumwandame juu. Ametangulia Bwana vitani, Twende mbele kwani ndiye amini.    Twende askari watu wa Mungu; Yesu yuko Mbele, tumwandame juu.    2. Jeshi la Shetani, likisikia Jina la Mwokozi, litakimbia, Kelele za shangwe zivume nchi; Ndugu inueni zenu sauti.   3. Kweli kundi dogo, watu wa Mungu Sisi na mababa tu moja fungu. Hatutengwi nao, moja imani, Tumaini moja, na moja dini.   4. Haya mbele watu nasi njiani, Inueni myoyo, nanyi sifuni; Heshima na sifa ni ya Mfalme, Juu hata chini, sana zivume. 

70 Yesu atuchunga

1. Yesu atuchunga, Mchunga wetu, Naye atufuta Machozi yetu; Mkononi mwake Hatuna hofu, Daima twapata Kwake wokovu.    2. Yesu atuchunga Tumemjua, Na sauti yake Twaitambua; Naye akituonya Ni kwa upole, Tu kondoo zake Hata milele.   3. Yesu atuchunga; Aliwafia Kondoo wakubwa Na wana pia; Kwamba awajua, Kondoo zake, Hutiwa alama Ya damu yake.   4. Yesu atuchunga; Mikono yake Imewaambata Kondoo zake; Hapati wadhuru Adui yule, Yesu awalinda. 

71 Mteteeni Yesu

1. Mteteeni Yesu, Mlio askari; Inueni beramu, Mukae tayari, Kwenda nae vitani, Sisi hatuchoki Hata washindwe pia Yeye amiliki.    2. Mteteeni Yesu, Vita ni vikali; Leo siku ya Bwana, Atashinda kweli, Waume twende naye, Adui ni wengi, Lakini kwake Bwana Tuna nguvu nyingi.   3. Mteteeni Yesu, Wenye ushujaa; Nguvu zenu za mwili Hazitatufaa; Silaha ya injili Vaeni daima, Kesheni mkiomba, Sirudini nyuma.   4. Mteteeni Yesu, Vita ni vikali, Wengi wamdharau, Hawamkubali, Ila atamiliki Tusitie shaka, Kuwa naye vitani Twashinda hakika. 

72 Twendeni! Haraka!

1. Twendeni! Haraka! Tupeleke Neno Liwe mwanga kwa nchi zilizo giza. Bwana alisema nendeni po pote Kawafundisheni mataifa yote. Pelekeni Injili kwa jina la Yesu. Upesi! Twendeni haraka!    2. Twendeni! Haraka! Tupeleke Neno La upendo wa Mungu kwa watu wote; Aliyeupenda sana ulimwengu Akamtoa Yesu Mwana wake pekee Kaleta wokovu, tumtangazeni. Upesi! Twendeni haraka!   3. Twendeni! Haraka! Tupeleke Neno La uzima kwa watu waliokufa. Mateka ya Shetani litafungua Litaponyesha na kuwapa amani. Twendeni upesi, tukawaokoe. Upesi! Twendeni haraka! 

73 Yesu zamani Bethilehemu

1. Yesu zama Bethilehemu, Aliyezaliwa kwa aibu, Ndiye mwakozi wa ulimwengu, Akaja kwa mimi.    Akaja kwa mimi; akaja kwa mimi; Ndiye mwaokozi wa ulimwengu, Akaja kwa mimi.  2. Yesu akafa msalabani, Kuniponya akalipa deni, Ni la ajabu ya jinsi gani Kunifia mimi!   Kunifia mimi! Kunifia mimi! Ni la ajabu ya jinsi gani Kunifia mimi.   3. Ni yeye huyo tangu asili; Na nilipotanga-tanga mbali Alikuja kwa upole, kweli Kuniita mimi.   Kuniita mimi; Kuniita mimi; Alikuja kwa upole, kweli Kuniita mimi   4. Yesu kristo atarudi tena, Hilo lanifurahisha sana. Yeye Bwana akionekana Kunijia mimi.   Kunijia mimi, kunijia mimi, Yeye Bwana akionekana Kunijia mimi 

74 Wachunga walipolinda

1. Wachunga walipolinda Kucha nyama zao, Malaika mtukufu Alishuka kwao.    2. Wakacha sana wachunga, Akawatuliza, “Nawaletea habari Ya kuwapendeza.”   3. ”Mji ule wa Daudi Leo amezawa Mwokozi ni Kristo Bwana, Ilivyoandikwa”.   4. ”Huyo mwana wa Mbinguni Ataonekana, Amelazwa kihorini Malazi hapana.”   5. Alipokwisha yanena Malaika hao Waliimba wimbo huu Usio na mwisho:   6. ”Enzi ni yake Munju juu, Na nchi salama, Kwa watu nao radhi kuu, Sasa na daima.” 

75 Waimba, sikizeni

1. Waimba, sikizeni, Malaika Mbinguni; Wimbo wa tamu sana Wa pendo zake Bwana, “Duniani salama, Kwa wakosa rehema.” Sisi sote na twimbe Nao wale wajumbe; Waimba, sikizeni, Malaika mbinguni.    2. Ndiye Bwana wa Mbingu, Tangu milele Mungu, Amezaliwa mwili, Mwana wa mwanamwali; Ametoka enzini Kuja ulimwenguni Mwokozi atufie, Ili tusipotee. Waimba, sikizeni, Malaika Mbinguni.   3. Mtukufu wa amani Ametoka Mbinguni, Jua la haki, ndiye Atumulikiaye; Amejivua enzi, Alivyo na mapenzi, Ataka kutuponya, Kutuzalisha upya, Waimba sikizeni, Malaika Mbinguni.   4. Njoo upesi, Bwana, Twakutamani sana; Kaa nasi, mwokozi Vita hatuviwezi; Vunja kichwa cha nyoka, Sura zako andika, Tufanane na wewe, Kwetu sifa upewe, Waimba, sikizeni, Malaika Mbinguni. 

76 Njoni, enyi wa imani

1. Njoni na furaha, enyi wa imani, Njoni Bethilehemu upesi ! Amezaliwa jumbe wa Mbinguni; Njoni tumuabudu, njonu tumuabudu, Njoni tumuabudu Mwokozi.    2. Mungu wa waungu, Mwanga wa mianga, Amekuwa radhi kuzaliwa; Mungu wa kweli, wala si kiumbe; Njoni tumuabudu, njonu tumuabudu, Njoni tumuabudu Mwokozi.    3. Jeshi la Mbinguni, Imbeni kwa nguvu, Mbingu zote na zijae sifa; Sifuni Mungu aliye Mbinguni; Njoni tumuabudu, njonu tumuabudu, Njoni tumuabudu Mwokozi.    4. Ewe Bwana mwema, twakubarikia, Yesu, utukufu uwe wako; Neno la Baba limekuwa mwili; Njoni tumuabudu, njonu tumuabudu, Njoni tumuabudu Mwokozi. 

77 Msalabani pa Mwokozi

1. Msalabani pa mwokozi, Hapo niliomba upozi, Akaniokoa mpenzi, Mwana wa Mungu.    Mwana wa Mungu, Mwokozi wangu, Akaniokoa mpenzi, Mwana wa Mungu.  2. Chini ya mti msumbufu, Niliomba utakatifu, Alinikomboa kwa damu, Mwana wa Mungu.   Mwana wa Mungu, Mwokozi wangu, Alinikomboa kwa damu, Mwana wa Mungu.     3. Aliniokoa dhambini, Ikawa kunikaa ndani, Aliponifia mtini, Mwana wa Mungu.   Mwana wa Mungu, Mwokozi wangu, Aliponifia Mtini, Mwana wa Mungu.   4. Damu ya Yesu ya thamani, Huniokoa makosani, Huniendesha wokovuni, Mwana wa Mungu.   Mwana wa Mungu, Mwokozi wangu, Huniendesha wokovuni, Mwana wa Mungu. 5. Hicho kijito cha gharama, Leo jivike kwa kuzama, Kwake uuone uzima, Mwana wa Mungu.   Mwana wa Mungu, Mwokozi wangu, Kwake uuone uzima, Mwana wa Mungu. 

78 Sioshwi dhambi zangu

1. Sioshwi dhambi zangu, Bila damu yake Yesu. Hapendezewi Mungu, Bila damu yake Yesu.    Hakuna kabisa Dawa ya makosa Ya kututakasa, Ila damu yake Yesu.    2. La kunisafi sina Ila damu yake Yesu. Wala udhuru tena, Ila damu yake Yesu.   3. Sipati patanishwa, Bila damu yake Yesu. Hukumu yanitisha, Bila damu yake Yesu.   4. Sipati tumaini, Bila damu yake Yesu. Wema wala amani, Bila damu yake Yesu.   5. Yashinda ulimwengu, Hiyo damu yake Yesu. Na kutufikisha juu, Hiyo damu yake Yesu.   6. Twaimba: Utukufu Una damu yake Yesu. Milele twaisifu, Hiyo damu yake Yesu. 

79 Msalaba wa aibu

1. Msalaba wa aibu, Ulinipa amani; Uliniondoa kifungoni, Nilimotesekea.    2. Ee, Mwokozi wangu, Yesu Nitamwendea nani? Najiweka msalabani, Nikaoshwe damuni.   3. Nakupenda Bwana Yesu, Kwa kunipenda kwako, Napendezwa nikutumikie Maisha yangu yote.   4. Usifiwe Bwana Yesu, Kwa ulivyonifia, Aleluya, nakushukuru, Uliyenikomboa.   5. Msalaba ulishinda Nguvu zake adui, Ili mimi nikombolewe, Niwe mwana wa Mungu. 

80 Wamwendea Yesu kwa kusafiwa

1. Wamwendea Yesu kwa kusafiwa, Na kuoshwa kwa damu ya kondoo? Je, neema yake umemwagiwa? Umeoshwa kwa damu ya kondoo?    Kuoshwa, kwa damu, Itutakasayo ya kondoo; Ziwe safi nguo nyeupe mno; Umeoshwa kwa damu ya kondoo?    2. Wamwandama daima mkombozi Na kuoshwa na damu ya kondoo? Yako kwa msulubiwa makazi, Umeoshwa kwa damu ya kondoo?    3. Atakapokuja Bwana –arusi Uwe safi kwa damu ya kondoo! Yafae kwenda mbinguni mavazi Yafuliwe kwa damu ya kondoo.   4. Yatupwe yaliyo na takataka, Na uoshwe kwa damu ya kondoo. Huoni kijito chatiririka Na uoshwe kwa damu ya kondoo?

81 Chini ya msalaba

1. Chini ya msalaba Nataka simama; Ndio mwamba safarini, Wa kivuli chema; Ni kweli kwa roho yangu Ni tuo kamili, Tatua mzigo wangu Wakati wa hari.    2. Hapa ni pema sana, Ni ngome kamili; Hapa yameonekana, Mapenzi ya kweli; Kama alivyoonyeshwa Yakobo zamani, Msalaba umekuwa Ngazi ya Mbinguni.   3. Na Yesu msalabani Walimkemea, Alikufa niokoke Niliyepotea; Naona ajabu sana Ya mambo mawili Jinsi alivyonipenda, Nisiyestahili.    4. Atakayeonana, Na Yesu Mbinguni, Njia yake aanzapo Ni msalabani; Wokovu upo hapa tu, Mwingine hapana, Kisha kuna furaha kuu Pamoja na Bwana. 

82 Sioni haya kwa Bwana

1. Sioni haya kwa Bwana Kwake nitang’ara! Mti wake sitakana, Ni neno imara!    Msalaba ndio asili ya mema, Nikatua mzigo hapo; Nina uzima, furaha daima, Njoni kafurahini papo.    2. Kama kiti chake vivyo Ni yake ahadi, Alivyowekewa navyo Kamwe havirudi.   3. Bwana wangu, tena Mungu Ndilo lake jina! Hataacha roho yangu Wala kunikana.   4. Atakiri langu jina, Mbele za Babaye, Anipe pahali tena Mbinguni nikae. 

83 Kwa wingi wa nyama

1. Kwa wingi wa nyama, Na sadaka pia, Hupata wapi salama, Kwondoa hatia?    2. Sadaka ni Yesu, Hwondoa makosa; Dhabihu mwenye jina kuu, Atanitakasa.   3. Kwa yangu imani, Nikuweke sasa Mkono mwako kichwani Kukiri makosa.   4. Roho yakumbuka Mambo ya mtini, Mzigo ulijitweka, Ndiyo yangu deni.   5. Deni hutanguka, Tukimuamini; Kwa damu tumeokoka, Twimbe furahani.