Posts

Showing posts from March, 2022

84 Niwonapo mti bora

  1. Niwonapo mti bora Kristo aliponifia Kwangu pato ni hasara Kiburi nakichukia.    2. Na nisijivune, Bwana Ila kwa mauti yako; Upuzi sitaki tena, Ni chini ya damu yako.   3. Tangu kichwa hata nyayo, Zamwagwa pendo na hamu, Ndako pweke hamu hiyo, Pendo zako zimetimia.   4. Vitu vyote vya dunia, Si sadaka ya kutosha; Pendo zako zinawia Nafsi, mali, na maisha. 

85 Ni mtu wa simanzi

1. Ni “Mtu wa Simanzi”, Mwana wa mwenye enzi Mwenye mengi mapenzi! Asifiwe Bwana Yesu!    2. Akawa matesoni, “Mungu mwana yakini Akatoka Mbinguni: Asifiwe Bwana Yesu!   3. Akapata dhihaka, Mzoea – mashaka Ndiye yetu sadaka: Asifiwe Bwana Yesu!   4. Tu wenye dhambi sana; Kwake dhambi hamna, Na Mungu twapatana: Asifiwe Bwana Yesu!   5. Alikufa mtini, Akalia dhikini, Sasa yuko Mbinguni: Asifiwe Bwana Yesu!   6. Punde atarejea, Yesu kutunyakua, Ndipo tutamwimbia: Asifiwe Bwana Yesu! 

86 Damu imebubujika

1. Damu imebubujika, Ni ya Imanweli, Wakioga wenye taka, Husafiwa kweli.    2. Ilimpa kushukuru Mwivi mautini; Nami nisiye udhuru, Yanisafi ndani.   3. Kondoo wa kuuawa, Damu ina nguvu, Wako wote kuokoa, Kwa utimilivu.   4. Bwana tangu damu yako Kunisafi kale, Nimeimba sifa zako; Taimba milele.   5. Nikifa tazidi kwimba Sifa za wokovu Ulimi ujaponyamaa Vumbini mwa ufu.   6. Bwana, umenikirimu Nisiyestahili Kwa damu yako, sehemu Ya mali ya kweli.   7. Nikubali kukwimbia, Mbinguni milele, Mungu nitakusifia Jina lako pweke. 

87 Deni ya dhambi ilimalizika

  1. Deni yangu ya dhambi, Yesu amelipa. Kwake msalabani Nilipewa uzima. Deni ya dhambi, Msalabani, Ilimalizikia, Ni huru kabisa.    2. Bwana Yesu asema, “Mwanangu dhaifu, Uwezo wa ushindi Hupatikana kwangu.”   3. Bwana, kweli naona, Nguvu zako pekee Huondoa ukoma, Niwe kipya kiumbe.   4. Sina wema moyoni, Nidai neema, Nakubali kabisa, Kwa damu kusafiwa.   5. Hata huko Mbinguni Miguuni pake, “Yesu alinifia,” Nitaimba milele. 

88 Ndiyo damu ya Baraka

  1. Ndiyo damu ya baraka ituoshayo wakosa, Kwake Bwana twaokoka, nasi twamsifu sasa; Nimestahili hukumu, siwezi kujitakasa; Nioshe katika damu, takuwa safi kabisa.    Safi kabisa; safi kabisa! Nioshe katika damu; Takuwa safi kabisa.    2. Yesu alivikwa miiba, na kuangikwa Mtini, Na maumivu si haba yaliyompata chini. Nataka kijito hicho niende kuoga sasa; Ndicho kinitakasacho, nami ni safi kabisa.   Safi kabisa; safi kabisa! Ndicho kinitakasacho, Nami ni safi kabisa.   3. Baba, kweli nimekosa, moyo wangu ni dhaifu; Dhambi ni nyingi kabisa, nipate wapi wokovu? Yesu kijitoni pako, naja naamini sasa; Nioshe kwa damu yako, takuwa safi kabisa.   Safi kabisa; safi kabisa! Nioshe kwa damu yako, Nami ni safi kabisa. 

89 Kwa Kalvari

  1. Muda mwingi nilipotea, Sikufahamu msalaba, Wala aliyenifilia, Kwa Kalvari.    Rehema bure na neema, Samaha nalo nilipewa, Ndipo aliponifungua Kwa Kalvari.    2. Kwa neno lake Bwana Mungu, Nilijiona mimi mwovu, Nikageuka na kutubu, Kwa Kalvari.   3. Yote kwa Yesu namtolea, Ndiye mfalme wa pekee sasa, Kwa furaha nitamwimbia, Wa Kalvari.   4. Jinsi pendo lilivyo kuu, Neema ilishushwa toka juu, Alitufanyia wokovu Kwa Kalvari. 

90 Aliteswa, aliteswa

1. Aliteswa, aliteswa, Msalabani Yesu aliteswa, Dhambi zangu ameziondoa, Mahali pangu aliumizwa.    2. Alikufa, alikufa, Msalabani Yesu alikufa, Kwa kifo chake nakombolewa, Kwa kuwa Yesu alinifia.   3. ’Kafufuka, ‘kafufuka, Kaburini Yesu alitoka, Nami nimewekwa huru pia, kwa kuwa Yesu alifufuka.   4. Yuko hai, yuko hai, Mbinguni anaishi Mwombezi, Daima huniombea mimi, Kwa kuwa Yesu adumu hai.   5. Atarudi, atarudi, Siku moja Yesu atarudi, Na tutamwonapo tutafurahi, Kwa kupelekwa kwake Mbinguni.   6. Sifa kwake, sifa kwake, Mbinguni na huimbwa milele, Kwa furaha, masifu, na shangwe, Tutamwimbia Yesu milele. 

91 Mapenzi yako yafanyike, Bwana

1. Mapenzi yako yafanyike, Wewe mfinyanzi, nami towe, Unifinyange upendavyo, Mimi tayari, naja kwako.    2. Mapenzi yako yafanyike, Unihoji dhambi zote, Unisafishe vya kimwili, Niinamapo Msalabani.   3. Mapenzi yako yafanyike, Mimi dhaifu, mimi mnyonge. Uwezo wote, kwako kweli, Sasa niponye, Ee, Mwokozi.   4. Mapenzi yako yafanyike, Natoa kwako vitu vyote, Maisha, mali, moyo, mwili, Vyote ni vyako, kweli, kweli.   5. Mapenzi yako yafanyike, Mapenzi yangu yavunjike, Ninakubali uwe Bwana, Ni mali yako, twaa kabisa.   6. Mapenzi yako yafanyike, Unitawale siku zote, Sura ya Yesu umba kwangu, Nijaze Roho nayo nguvu. 

92 Nataka nimjue Yesu

  1. Nataka nimjue Yesu, Na nizidi kumfahamu, Nijue pendo lake, na Wokovu wake kamili.    Zaidi, zaidi, nimfahamu Yesu, Nijue pendo lake, na wokovu wake kamili.    2. Nataka nione Yesu, Na nizidi kusikia, Anenapo kitabuni, Kujidhihirisha kwangu.   3. Nataka nifahamu, na Nizidi kupambanua Mapenzi yake, nifanye Yale yanayompendeza.   4. Nataka nikae naye, Kwa mazungumzo zaidi, Nizidi kuwaonyesha Wengine wokovu wake.    Shared from Tenzi za Rohoni app. Click this link to download https://goo.gl/9HNM1M

93 Bwana amefufuka

1. Bwana amefufuka, Aleluya. Twimbe na malaika, Aleluya. Sifa zetu na shangwe, Aleluya. Na zao zisitengwe, Aleluya.    2. Ukombozi timamu, Aleluya. Umetimu kwa damu, Aleluya. Mshindi asifiwe, Aleluya. Yu hai kwa milele. Aleluya.   3. Jiwe, lindo, muhuri, Aleluya. Vi wapi? Na kaburi? Aleluya. Kifo hakimuweki, Aleluya. Ametoka peponi, Aleluya.   4. Yu hai mtukufu; Aleluya. Cha kifo hatuhofu! Aleluya. Alitufia sisi, Aleluya. Tuwe mahuru nasi, Aleluya.   5. Kichwa chatangulia, Aleluya. Tupae, nasi, pia!, Aleluya. Kwa kuwa tuna fungu, Aleluya. Mti, kaburi, mbinguni, Aleluya.   6. Ndiwe Mwokozi wetu, Aleluya. Sifa ni yako Yesu, Aleluya. Utukuzwe pekeo, Aleluya. Ni wewe ufufuo, Aleluya. 

94 Siku ya mbingu kujawa na sifa

1. Siku ya Mbinguni kujawa na sifa, Dhambi zilizidi duniani; Yesu akaja azaliwe mtu, Awe na watu ulimwenguni.    Alinipenda, alinifia, Ameondoa na dhambi zangu; Alifufuka nipewe haki, Yuaja tena Mwokozi wangu.    2. Na siku moja walikwenda naye, Wakamkaza msalabani; Aliumia, aliaibishwa, Ili atuokoe dhambini.   3. Siku hiyo wakamlaza chini Kaburini alipumzika; Matumaini yetu wenye dhambi, Ni mwokozi, kwake twaokoka.   4. Kaburi likashindwa kumshika; Jiwe likatoka mlangoni, Alifufuka kwa kushinda kwake, Naye yuko milele Mbinguni.   5. Siku moja atatujia tena; Utukufu wake tutaona; Atawaleta na wapenzi wetu; Mwokozi: wangu, tutaonana. 

95 Hivi vita vimekoma

  Aleluya! Aleluya! Aleluya!   1. Hivi vita vimekoma, Vimeshindwa na uzima, Na asifiwe daima, Bwana Yesu.    2. Nguvu za kifo ni hizo, Ila hazina uwezo, Ndizo sasa avunjazo, Bwana Yesu.   3. Siku tatu za huzuni, Kisha atoka ufuni, Asifiwe duniani, Bwana Yesu.   4. Mapingu ameyavunja, Mbingu amezifungua, Nasi sasa twamwimbia, Bwana Yesu.   5. Na ulivyopigwa wewe, Ni kwamba tufunguliwe, Milele na usifiwe, Bwana Yesu. 

96 Mle kaburini, Yesu mwokozi

1. Mle kaburini, Yesu Mwokozi! Alilazwa chini, Bwana wangu!    Bwana! Amefufuka, Kifo kimeshindwa kabisa! Gizani mle alitoka chini, Sasa atawala huko Mbinguni! Yu hai! Yu hai! Bwana Yesu yu hai!    2. Aungoja huo, Yesu Mwokozi! Mchana ujao, Bwana wangu!   3. Walinda kaburi, Yesu Mwokozi! Bure ni muhuri, Bwana wangu!    4. Kifo kimeshindwa, Yesu mwokozi! Pingu zimevunjwa, Bwana wangu! 

97 Tazameni huyo ndiye

1. Tazameni huyo ndiye, Mwenye kushinda vita; Haya, tumsujudie; Nyara anazileta; Watu wote msifuni, Sasa yumo kitini.    2. Msifuni malaika, Mtukuzeni sana, Wote waliookoka Watamsifu Bwana; Watu wote msifuni, Sasa yumo kitini.   3. Walimfanya dhihaka Zamani wenye shari, Kwao waliookoka Ni Bwana wa fahari; Watu wote msifuni. Sasa yumo Kitini.   4. Nyimbo nzuri, sikizeni, Ni nyimbo za sifa kuu, Za Bwana Yesu kitini, Kutawazwa, yeye tu; Watu wote msifuni Sasa yumo Kitini. 

98 Huyo ndiye anashuka

1. Huyo ndiye! anaskuka, Aliyetufilia, Wengi waliookoka, Wakimfurahia, Aleluya! Yesu aturudia.    2. Sote tutamtazama, Amekaa kitini, Nao waliomcoma, Kumkaza mtini, Na kilio, wamuone enzini.   3. Alama za kifo chake Hata sasa anazo Na waaminifu wake Wapendezewa nazo. Alipata, Kwetu alama hizo.   4. Wokovu utakiwao Sasa wapatikana, Na watakatifu hao Mbinguni wakutana Kumlaki, Ndiyo siku ya Bwana   5. Wakusujudie wote Mbele ya kiti chako. Zako, Bwana, nguvu zote Itwae milki yako Njoo Bwana, Sisi tu watu wako. 

99 Maelfu na maelfu

1. Maelfu na maelfu Wenye nguo bora! Masafu ya waongofu Wenye na bendera! Amekwisha kamili Vita vya shetani Fungueni lango hili; Njoni, ingieni!    2. Imbeni aleluya, Zipae Mbinguni! Pigeni sana sauti Kwa kutumaini! Kwa hiyo viliumbwa Nchi hata Mbingu Dhiki za muda zikisha, Asifiwe Yesu.   3. Loo! Tukionana Pwani ya ng’amboni! Loo! Tukishirikiana Milele Mbinguni! Midomo yote pia, Huko itaimba Wajane kufufukiwa Na kila yatima!   4. Himiza enzi yako, Uliyetufia Utimize watu wako, Wakosaji pia, Mpendwa wa taifa twakutumaini! Uzifunue ishara Urudi enzini!