Posts

Showing posts from December, 2021

150 Haya, ee moyo wangu

1. Haya ee moyo wangu, imba kwa furaha. Umwimbie Muumbaji mbingu na dunia. Atukuzwaye pote umsifu na wewe kwa nguvu zako zote, umri wako wote.   2. Mungu wake Yakobo. ndiye Mungu wwetu. Ukimchagua yeye, una fungu jema, unacho kitu chema, umepata mali; moyo utakung’aa shida zitakwisha.   3. Ni mwenye nguvu nyingi, hana amshindaye, kwa hekima aumba vyote ni ajabu, misitu na mabonde, milima,mashamba, vilivyo baharini wanyama porini.   4. Ana mizungu mingi, kuponya wanawe. Anawapa riziki, hata siku za njaa. Wenye chakula haba wanenepa miili: hata waliofungwa anawafungua.   5. Mashangilio yote hayamtoshi yeye. Ni mwema peke yake nami ni vumbi tu! Ananihurumia kwa kuwa ni wake, kwa hiyo nalikuza Jina lake pote.

151 Usiku mtakatifu

1. Usiku mtakatifu! Wengine walala Wakeshao ni Yosefu tu na Maria waliomlinda Yesu mwana mzuri Yesu mwana mzuri   2. Usiku mtakatifu! Wachunga wapewa habari nzuri na malaika, zienezwe popote sasa: Yesu Mponya kaja Yesu Mponya kaja.   3. Usiku mtakatifu! Siku ya furaha imetuangaza Kimungu tumepewa ukombozi Kristo amefika Kristo amefika.  

152 Uliyesulibishwa

1. Uliyesulubishwa, Mtakatifu Bwanangu, Uwe ngao shidani, uniombee mimi. Uliyesulubishwa, Mtakatifu Bwanangu!   2. Wongofu sina hata, niondolee makosa. Mwovu akinishtaki nasumbuka rohoni. Wongofu sina hata, niondolee makosa.   3. Wewe tu nipokee, nakukumbilia wee. Hata nifanye bidii, nikatoe machozi. Wewe tu nipokee, nakukimbilia wewe   4. Uwe ngao shidani, Niombee na mimi! Hapa nikiumizwa, Saa ya mwisho ikija: Uwe ngao shidani, Niombee na mimi!

153 Nimepita ulimwengu

1. Nimepita ulimwengu, ulimwengu ni mzuri, lakini natamani ulimwengu mwingine.   2. Nimeona watu wengi, hutafuta daima Maisha yao yote, ndiyo taabu na shida.   3. Imebaki hali njema ya furaha ya roho: Hubirini popote; taabu itatulia.   4. Msalabani pa Golgota jerahani mwa Yesu ni mahali penye raha kwao wote kabisa.  

154 Bariki yote yawe mema

  1. Bariki yote yawe mema, yote yawe mbaraka. Watu wa nchi za duniani, uwajaze utukufu.   Kaa kwetu, Bwana, bariki. Uamini wee ee ndugu kweli yake Kristo. Jaa utukufu wa Bwana siku zako zote. Vaa Mwokozi ee na kweli yake, Haleluya.   2. Nyumba za wote zibariki kwa Jina lako takata. Ujaze utukufu wako, nchi zote dunia, Kaa kwetu, Bwana…   3. Nyosha mkono ubariki, waliojiunga nawe. Wakupokee maishani, watunzwe nawe milele. Kaa kwetu, Bwana…..   4. Bwana yatunze mambo yote yaliyo mazuri kwako Uwape wote wakuombao, wafanikishe maisha. Kaa kwetu Bwana….

155 Hapana rafiki kama Yesu

  1. Hapana rafiki kama Yesu, Yu pekee, Yu pekee; Hapana mpozi kama Yesu Yu pekee, Yu pekee.   Yesu ajua shida zetu, Aweza kutuongoza; Hapana rafiki kama Yesu, Yu pekee yu pekee.   2. Yeye anaye sifa, ni Yesu Yu pekee, yu pekee; Ndiye aliye mnyenyekevu Yu pekee, yu pekee; Yesu ajua……   3. Yesu pamoja nasi daima, Yu pekee, yu pekee; Kwa usiku aleta salama, Yu pekee, yu pekee; Yesu ajua……   4. Kulinda Yesu yu Mwaminifu, Yu pekee, yu pekee; Atawakubali wahalifu, Yu pekee, yu pekee; Yesu ajua…..   5. Alipelekwa awe mwokozi, Yu pekee, yu peee; Anatutayarisha enzi Yu pekee, yu pekee; Yesu ajua…….  

156 Bwana Yesu yuko wapi

1. Bwana Yesu yuko wapi, Mpenzi wangu rafiki? Njia gani amekwenda? Nitamwonaje mimi? Roho yangu yajutishwa Na dhambi na huzuni; Yesu mpenzi wangu Mwema Namtafuta kwa bidii.   2. Ninapaza sauti yangu Nalia:wapi Yesu? Ndani mwangu sina raha Mpaka nimwone Yesu. Ningekuwa na mabawa Ningeruka upesi Milimani, mabondeni Kumtafuta Bwanangu   3. Aondoa shida zangu, Maharibifu yote. Nikiona taabu mimi Anituliza yeye. Nitafanya bidii sana; Kumtafuta popote; Sitachoka kutembea Mchana hata usiku.   4. Bwana Yesu nitokee, Roho inakuita. Niondoe na maovu Yesu mwokozi wangu. Utilize hamu yangu Kaa kwangu daima. Nikupende sana wewe, Niwe wako milele.  

157 Kijito cha utakaso

  1. Kijito cha utakaso ni damu ya Yesu, Bwana anao uwezo kunipa wokovu   Kijito cha utakaso, Nizame kuoshwa humo Namsifu Bwana kwa hiyo Nimepata utakaso   2. Viumbe vipya naona; damu ina nguvu, imeharibu uovu ulionidhulumu   3. Naondoka kutembea nuruni mwa mbingu, Na moyo safi kabisa kumpendeza Mungu.   4. Ni neema ya ajabu kupakwa na damu; na Bwana Yesu kumjua Yesu wa Msalaba.

158 Aniongoza po pote

1. Aniongoza popote NimwandameSiku zote Mapenzi yake ni heri Yalitimizwa kalvari.   2. Nitaongozwa na Bwana Usiku kucha na mchana Yesu rafiki wa heri Ninakumbuka kalvari.   3. Lanitosha neno lake Nishikwe na mkono wake Mapenzi yake ni heri Yalitimizwa kalvari   4. Nitaendelea mbele Pamoja naye milele Pendo lake ni hiyari Bwana Yesu wa Kalvari

159 Ushirika mkuu, furaha yangu

1. Ushirika mkuu, furaha yangu, Kumtegemea Bwana Yesu, Nina baraka, amani pia, Kumtegemea Bwana Yesu.   Raha, Raha, Nina raha na salama, Raha, Raha, kwa kumtegemea Yesu.   2. Ni halisi kutembea naye, Kwa kumtegemea Yesu. Naona nuru njiani mwangu, Kumtegemea Bwana Yesu.   3. Sioni shaka wala hasara, Kumtegemea Bwana Yesu; Nina amanikwake Mwolozi, Kumtegemea Bwana Yesu.

160 Jioni moyo wangu

  1. Jioni moyo wangu wakutafuta Bwana, na kukushukuru. Unikazie macho yenye baraka nyingi, ung’aze mwili na roho.   2. Natumaini tena rehema yako Baba hata usiku huu. Fukuza majaribu na hila ya shetani, ukiwa karibu yangu   3. Unanipenda sana, wakaa pamoja nami, wanikaribisha. Unanifurahisha kwa wema wako mwingi, sababu hii nakusifu.   4. Maisha yanapita upesi, ni safari ya kwenda mbinguni. Unifundishe, Bwana, kuelekea kwako: Pazuri ni mbinguni tu.

161 Usiku uingiapo

1. Usiku uingiapo, umwaze Mungu Mkuu, aendeshaye dunia kwa mwendo mtulivu.   2. Kwa nini wahangaika usiku namchana? Umtwishe huzuni yako aliyekuumba.   3. Kwake haujapunguka uwezo na msaada. Atayatimiza yote aliyoyaanza.   4. Ukamwachie kutenda atakalo kwako! Kwa hiyo ulale raha na kufurahiwa.